Wahamiaji Haramu: Kuna siku Tanzania itatawaliwa na mgeni
Baptista Marco raia wa Burundi aliyekamatwa nchini hivi karibuni akifanya kazi kama mwanasheria wa TBS kinyume cha sheria. Matukio ya wageni kukamatwa wakifanya kazi nchini–tena nyingine nyeti–kinyume cha sheria yanazidi kuongezeka kiasi cha kuanza kujenga shaka juu ya usalama wa taifa na wananchi kwa ujumla. Hapa lazima tujiulize tatizo liko wapi; na nini kifanyike kuondoa hatari hii ambayo inaweza kutugharimu kama taifa. Wahenga walinena: usipoziba ufa, utajenga ukuta; jambo ambalo ni gharama baada ya nyumba kubomoka. Kuna matukio ambapo wakimbizi wa kiuchumi wa kigeni wamemeajiriwa nchini na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kustukiwa. Je vyombo vyetu wa usalama vinafanya kazi gani na kama vinafanya kazi je vinaifanya vizuri? Mtu anaajiriwa kwa ngazi ya juu. Je anapataje kazi kama hakuna rushwa? Je wako wangapi wahalifu wa namna hii? Je wako peke yao au wan...