Posts

Showing posts from December 19, 2017

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 19,2017

Image
Magazetini leo Jumanne December 19 2017

HALI YA UZALISHAJI UMEME VITUO VYA PANGANI HYDRO SYSTEM VIKO KATIKA HAKLI NZURI; MHANDISI MAHENDA

Image
Mhandisi Mahenda S. Mahenda, Meneja wa Vituo vya  uzalishaji umeme wa maji vya Pangani  Hydro Systems,  vinavyohusisha  inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Korogwe VITUO vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani  Hydro Systems , ambayo inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97, viko katika hali nzuri, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S. Mahenda, amesema Leo Desemba 18, 2017. Hata hivyo amesema, mashine moja kati ya mbili kwenye kituo cha Hale, haifanyi kazi na iko katika matengenezo. “Niwahakikishie tu kwamba matengenezo hayo ambayo bado hayajaanza hayataathiri upatikanaji umeme kwa sababu vyanzo vya umeme vimeongezeka.” Alisema. Akif...

EPL: Klabu gani ina wakati mgumu zaidi msimu wa Krismasi?

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Ilichukua siku 87 kucheza mechi 11 za kwanza Ligi ya Premia. Lakini mechi 11 zinazofuata zitachezwa katika siku 47 pekee. Kila moja kati ya klabu zilizo kwenye Ligi Kuu itacheza mechi nne wakati wa sikukuu - mechi moja zaidi ya msimu uliopita. Msimu uliopita, kila klabu ilikuwa na wiki ya kupumzika kabla ya mechi za Boxing Day isipokuwa Everton. Mwaka huu, Leicester City watacheza mechi nne - kati ya 23 Desemba na 1 Januari - kipindi cha saa 213. West Ham, nao watacheza mechi zao nne kwa mwendo wa aste aste kiasi, saa 294 na dakika 45. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Msimu huu klabu ya Arsene Wenger ina nafuu zaidi ya klabu nyingine Hii ni baada ya mechi yao ya Mkesha wa mwaka Mpya dhidi ya Tottenham kuhamishwa hadi 4 Januari kwa sababu za kiusalama. Hilo limewapa karibu siku tatu za ziada za kupumzika. Je, mpangilio kwa klabu mbalimbali ukoje? Pamoja na Arsenal, mabingwa watetezi Chelsea pia wana mpangilio...

Trump: China na Urusi ndio washindani wakubwa wa Marekani

Image
Image caption Rais Trump Rais Donald Trump ametangaza mkakati wa kitaifa wa usalama katika utawala wake ambao unaangazia vipaumbele vya kwanza vya Marekani. Mkakati huo umesisitiza ukuaji wa kiuchumi na usalama wa taifa hilo kwa kuweka sheria kali za kulinda mipaka na kuwa na jeshi imara. Katika hotuba yake,rais Trump ametaja kuwa China na Urusi ni washindani wanaopinga ushawishi wa Marekani katika ngazi ya kimataifa. Licha ya kuwa Marekani inaongoza kwa kuwa na jeshi lenye nguvu lakini bado wapinzani wake wa kisiasa na kiuchumi wanahangaika duniani kote ili kuitoa katika mstari. Huku ikiwa inakabiliwa na makundi ya kigaidi ,mitandao ya wahalifu na watu wengine ambao wanachochea vurugu na uovu. Aidha mkakati huo unajumuisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Mexico, kuimarisha sheria za uhamiaji na kusitisha mpango wa kutoa viza za bahati nasibu. Trump pia aliwakosoa pia Marais waliopita wa Marekani akisema wameshiriki katika ujenzi wa mataifa ya nje badala ya kuendelez...

Marekani yailaumu Korea Kaskazini kwa kirusi cha WannaCry

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Thomas Bossert ambuye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyesama haya kupitia jarida la Wall Street Journal. Utawala nchini Marekani unasema kuwa Korea Kaskazini ilihusika moja kwa moja na kirusi cha wannaCry kilichoadhiri hospitali, biashara na mabenki kote duniani mapema mwaka huu. Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola. Thomas Bossert ambaye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyasema haya kupitia jarida la Wall Street Journal. Hii ndiyo mara ya kwanza Marekani imeilaumu Korea Kaskazimni kwa kirusi hicho. Haki miliki ya picha EPA Image caption Kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo. Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompiuta ya...

Cyril Ramaphosa ndiye kiongozi mpya wa chama cha ANC, Afrika Kusini

Image
Image caption Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini A-Kusini . Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini A-Kusini . Ramposa ambaye alikuwa makamu wa rais wa chama hicho aliweza kumshinda mpinzani wake Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura 2440 kwa 2161. Kwa sasa Ramaphosa ameoneka kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019. Hata hivyo Cyril Ramposa amekuwa kiongozi wakati ambao Afrika kusini inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinafanya mambo hayendi sawa katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika . Cyril Ramaphosa ni mtu wa aina gani? Cyril Ramposa alizaliwa tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio mwanasiasa tajiri zaidi Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni dola milioni 450.Tangu ujana wake Ramposa alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa shupavu na hiyo ndio ilimfanya kujiunga na uongo...

MTOTO WA GADDAFI KUGOMBEA URAIS MWAKANI

Image
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi, anatarajia kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2018. Taarifa za Saif al-Islam kutaka kugombea nafasi hiyo ambayo baba yake alikuwa ameishikilia kwa muda wa miaka 42, ilitolewa na msemaji wa familia Basem Hashimi Soul. “Saif al-Islam atagombea urais kwenye uchaguzi ujao ambao unaweza ukafanyika katikati mmwa mwaka 2018,ana dhamira ya kuongeza ulinzi zaidi na utulivu kulingana na jografia ya Libya, kwa kushirikiana na makundi yote ya Libya, hivi karibuni anatarajia kuweka wazi tarahe ya kujitangaza rasmi kwenye vyombo vya habari”, amesema msemaji Basem Hashimi Soul. Nchi ya Libya hivi karibuni imekuwa isiyo ya utulivu, kutokana na vurugu zinazoendelea, huku mtoto huyo wa Gaddafi akiwa na imani kubwa Umoja wa Mataifa utakubaliana nae katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi hiyo kinaipitia, cha kutafuta utulivu. Saif al-Islam ni mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi ambaye alitolewa madarakani...

Nassari Aishangaa TAKUKURU Kutupa Ushahidi Wake

Image
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshangazwa na Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa kushindwa kuona uhalisia au uongo kwenye ushahidi waliouwasilisha dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti na badala yake,wameona siasa. Nassari amesema hayo ikiwa ni siku moja kupita baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi wao kwa kudai kwamba uliharibiwa kwa kuingiza siasa. Nassari amesema kwamba “Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka. Cha ajabu hawajaona uhalisia au uongo uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi," Nassari. Nassari amefafanua kwamba katika kuwasilisha ushahidi wa kununuliwa kwa madiwani aliwakabidhi moja ya kifaa alichotumia kurekodia baadhi ya matukio. "Niliwapa takukur...