Posts

Showing posts from August 25, 2015

Magufuli Akataa Kumia Helikopta.......Asema Atatumia Gari ili Azijue Kero za Wananchi

Image
MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema katika sehemu kubwa ya kampeni yake, atatumia zaidi usafiri wa barabara ili apate fursa ya kuzijua kwa karibu kero za wananchi katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, alifafanua kuwa kwa maeneo mengine yenye ulazima wa kutumia usafiri mbadala, anaweza kufanya hivyo, lakini dhamira yake ni kutumia zaidi barabara. Aidha, amezitaja sifa ya waziri ajaye wa ujenzi, ambaye atarithi wizara aliyoitumikia kwa miaka 15, iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza tangu kuzinduliwa kwa kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Mishamo, kilichopo Kilometa 150 kutoka mkoani Katavi, Dk Magufuli alisema amekataa kutumia helikopta katika baadhi ya sehemu atakazofanya ziara, ili kujionea mwenyewe kero ya barabara inayowakabili Watanzania. Moja ya barabara alizoahidi kujenga ni pamoja na kutoka Tabora mpaka Mpanda, ambayo ina kilometa zaidi ya 356 na ya Mpand...

11 Mbaroni kwa Tuhuma za Kuchoma Moto Kituo cha Polisi Morogoro

Image
                       Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo. POLISI mkoani Morogoro wanashikilia watu 11, wakazi wa Kijiji cha Mpofu wilayani Kilombero kwa tuhuma za kuvamia na kuchoma moto kituo kidogo cha polisi na ofisi ya serikali ya kijiji hicho. Watuhumiwa hao ni sehemu ya zaidi ya watu 100 wanaodaiwa kufanya uhalifu huo katika kituo hicho cha polisi Mbingu, katika taarifa ya Mgeta. Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo wakishinikiza polisi wamwachie mtuhumiwa aliyewekwa mahabusu katika kituo hicho, Bashiri Kadugula (25), kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Veronica Chabula (21) ili wamwadhibu. Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema jana kuwa, Kadugula aliwekwa ndani kwa kumkata mkewe kwa panga sehemu mbalimbali za mwili kutokana na wivu wa mapenzi. Alisema katika tukio hilo ni la Agosti 20...