“SITAKI KUONA KIONGOZI WA DINI ANASUMBULIWA”- RC MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewataka Viongozi wa Dini zote Waislam na Wakristo wenye matatizo yanayohitaji msaada wa Serikali ikiwemo Migogoro na Kesi kufika Ofisi kwake ili yaweze kupatiwa ufumbuzi. RC Makonda amesema hayo wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kanisa la KKKT Ubungo iliyoenda sambamba na Jubilee ya Miaka 500 ya Ujenzi wa Kanisa. Amesema kuwa Viongozi wa Dini wanafanya kazi kubwa ya kiroho katika kuijenga Jamii Bora hivyo hawapaswi kuzungushwa na Watendaji wa Serikali pale wanapohitaji kuhudumiwa kwakuwa thamani ya kazi wanayoifanya ni kubwa. “Mimi sio Mkuu wa Mkoa bali mimi ni Mtumishi wa Mungu katika Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam, Niwaombe Viongozi wote wa Dini Dar es Salaam sasa hivi msiangaike mkiwa na kesi kwenda kwa Wenyeviti wa Mtaa au Watendaji wa Mtaa, mkiwa na tatizo lolote njooni Ofisin kwangu, mimi ndio nitawatafuta hao, nisingependa kuona Kanisa au Msikiti wanasumbuliwa na Migogoro isiyoeleweka kwa misingi ya watu fula...