Zanzibar kunani??Simba nayo yawasili Unguja, Yanga yatimkia Pemba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani
M chezaji wa timu ya Simba ya Dar aliyesainiwa kutoka wahasimu wa jadi Yanga, Haruna Nyiyonzima alipowasili katika Bandari ya Unguja jana mchana Wachezaji wa timu ya Simba ya Dar walipowasili katika Bandari ya Unguja jana mchana Kocho Mkuu wa timu ya Simu Omog akiwa akisubiri usafiri wa kuwapeleka Hoteli ya Mtoni Marine watakaapofikia wakati walipowasili katika Bandari uya Unguja jana mchana Wachezaji wa timu ya Simba ya Dar walipowasili katika Bandari ya Unguja jana mchana Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar. Kikosi cha wachezaji 23 cha Simba kimewasili Visiwani Zanzibar jioni ya leo wakitokea Jijini Dar es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao leo asubuhi waliondoka Unguja na kwenda Pemba kwaajili ya kambi pia. Simba wataweka kambi visiwani hapa mpaka Agosti 22, 2017 siku moja kabla ya mchezo wao utakaopigwa Agosti 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar...