Posts

Showing posts from December 17, 2017

Nini siri ya mafanikio ya CCM Tanzania?

Image
Haki miliki ya picha AFP/GETTY Shughuli ya kusukwa upya kwa safu ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania itahitimishwa wiki hii katika mkutano mkuu unaofanyika mjini Dodoma, katikati mwa nchi hiyo. Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu Rais John Magufuli aliporithi uenyekiti kutoka kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete.  CCM inaendeleza mikakati ya kurejesha hadhi yake baada ya ushindi uchaguzi wa mwaka 2015. Licha ya kushinda urais kwa taabu, wapinzani chini ya mwamvuli wa UKAWA walipata karibu theluthi moja ya viti vyote vya ubunge na kudhibiti halmashauri katika miji muhimu ikiwemo Dar es Salaam, hii ikiwa ni rekodi mpya.  Miaka miwili ndani ya utawala wa Rais Magufuli, upepo unaonekana kugeuka. Upinzani unaelekea kudhoofika, wakati CCM ikiimarika na kung'ara miongoni vyama vya ukombozi vilivyoleta uhuru katika nchi zao.  Ingawa haikuwepo wakati wa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 wala mapinduzi ya Zanzibar 1964, CCM inahesabika kama chama cha uko...