Posts

Showing posts from November 20, 2017

Juventus wachapwa baada ya kumpumzisha Gianluigi Buffon

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Gianluigi Buffon (kati) amecheza mechi 627 Serie A , 20 nyuma ya rekodi ya Paolo Maldini Gianluigi Buffon aliachwa kwenye benchi Juventus walipokuwa wanacheza dhidi ya Sampdoria, hatua ambayo huenda iliwagharimu Jumapili. Walipokezwa kichapo cha 3-2. Buffon aliwekwa kwenye benchi pamoja na beki Andrea Barzagli, kwa sababu wanahitaji "muda kusahau" masaibu ya kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia. Massimiliano Allegri aliwapumzisha wawili hao, ambao tayari wamestaafu soka ya kimataifa, baada ya Italia kushindwa na Sweden mechi za muondoano wa kufuzu. Sampdoria waliongoza kupitia bao la kichwa la Duvan Zapata, Lucas Torreira na Gianmarco Ferrari nao wakaongeza na kufanya mambo 3-0. Gonzalo Higuain na nguvu mpya Paulo Dybala walikomboa mawili dakika za mwisho. Juventus wamesalia alama nne nyuma ya viongozi wa ligi Napoli ambao bado hawajashindwa. Inter Milan waliwapiku na kuingia nafasi ya pili baada ya kuwashinda At...

Benevento wavunja rekodi ya Manchester United

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Benevento walikuwa tayari wamevunja rekodi ya kuwa na mwanzo mbaya zaidi Serie A Klabu ya Benevento nchini Italia imevunja rekodi ya Manchester United ya kuwa klabu iliyoanza msimu vibaya zaidi katika ligi mojawapo kati ya ligi tano kuu za soka Ulaya. Hii ni baada ya klabu hiyo kulazwa 2-1 muda wa ziada na Sassuolo. Limbukeni hao wa Serie A wameshindwa mechi zao 13 za kwanza kwenye msimu na hivyo wakavunja rekodi ya United ambao walishindwa mechi 12 mwanzo wa msimu wa 1930-31. Alessandro Matri aliwaweka Sassuolo kifua mbele lakini Samuel Armenteros akasawazisha kabla ya Gaetano Letizia alioneshwa kadi nyekundu upande wa Benevento. Domenico Berardi alipoteza penalti upande wa Sassuolo kabla ya Federico Peluso kuwafungia bao la ushindi. Benevento, ambao walifanikiwa kurejea Serie A mtawalia, walidhani wangepata alama yao ya kwanza ya msimu pale mkwaju wa penalti wa Berardi ulipogonga mwamba na kukosa kuingia. Matumaini yao...

Kansela Merkel awekwa njia panda

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Mazungumzo kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani yamevunjika, hali ambayo inaweka njia panda mstakabali wa Kansela Angela Merkel. Baada ya wiki nane ya majadiliano chama chenye mrengo wa kati cha Centrist Free Democrats -FDP- kimejitoa kikilalamikia tofauti zisizoweza kusuluhishwa na chama cha Merkel cha Christian Democrats na vyama vingine katika mazungumzo. Baadaye leo bibi Merkel atakutana na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, ambaye ndiye mwenye nguvu kuitisha uchaguzi mpya. Bibi Merkel ameonya kuwepo kwa magumu katika wiki zijazo. Kiuhalisia makubaliano9 ya muungano huo yanawezekana lakini bado haijawa wazi iwapo kuna uwezekano wowote washiriki kufanya umuhimu wa kupata suluhu.

Mahakama ya Kenya kuamua juu ya kesi ya urais leo

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji Mkuu wa Mahakama ya juu zaidi nchini kenya David Maraga Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya Jumatatu inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi zilizowasilishwa kwenye mahakama hiyo kupinga uchaguzi wa marudio wa tarehe 26 Oktoba ambapo rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitangazwa kama mshindi.  Katika  K esi majaji watatakiwa kutoa uamuzi kuhusu masuala yafuatayo: Wataamua iwapo tume huru ya taifa ya chaguzi na mipaka (IEBC ) ilifaa kuteuwa upya wagombea urais au la. Uamuzi pia utatolewa na mahakama hiyo juu zaidi juu ya ya ikiwa kujiondoa kwenye uchaguzi huo kwa kiongozi Muungano wa upinzani Raila Odinga na Makamu wake Kalonzo Musyoka kuliathiri uchaguzi huo. Majaji pia watatoa uamuzi kuhusu ikiwa baada ya tume ya IEBC kushindwa kuendesha uchaguzi katika ameneo bunge 25 kati ya 290 kunahalalisha ama kubatilisha matokeo ya uchaguzi. Aidha Mahakama hiyo itawaeleza waKenya ikiwa tume ya uchaguzi (IEBC) ilikuwa na uwezo wa kuandaa uch...

Chama tawala cha Zimbabwe ZANU - PF kumshtaki Mugabe

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Rais Robert Mugabe akihutubia taifa Jumapili usiku Mtandao wa Twitter unaofuatilia taarifa za vyombo vya habari nchini Zimbabwe unaripoti kuwa Kiongozi wa chama tawala Cha ZANU PF anaamini mchakato wa kumshtaki Bwana Mugabe utaendelea kama ilivyopangwa Jumanne , wakati ambapo chama bunge linatarajiwa kukaa.  Hii ni kama muda wa makataa uliowekwa wa kujiuzulu kwake ambao ni Jumatatu saa sita adhuhuri utakwisha kabla Bwana Mugabe hajajiuzulu Halikuwa tangazo ambalo baadhi ya waZimbabwe walilisubiri. Bwana Mugabe bado ni rais na haijawa wazi ikiwa bunge sasa litaanza mchakato wa kumshitaki. Haki miliki ya picha AFP Image caption Raia wa Zimbabwe wakirekodi hotuba ya kujiuzulu kwake Watu wa Zimbabwe walikuwa wanatarajia kusikia mugabe akijiuzulu kulingana na madai yao. Baadhi ya wale waliokusanyika kufuatilia hotuba yake kwenye vilabu waliiambia BBC kuwa wamekatishwa tamaa na kutojiuzulu kwa rais Mugabe. Hata hivyo hali ya imeend...

Mugabe akataa kuachia madaraka Zimbabwe licha ya shinikizo

Image
Haki miliki ya picha STR/AFP/GETTY Image caption Wengi walitarajia kwamba Robert Mugabe angetangaza kujiuzulu Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameapa kuendelea kuongoza taifa hilo kwa wiki kadha, licha ya shinikizo kutolewa kumtaka aachie madaraka. Akihutubu moja kwa moja kupitia runinga ya taifa, Bw Mugabe amesema anapanga kuongoza mkutano mkuu wa chama mwezi Desemba. Maafisa wakuu wa chama hicho cha Zanu-PF walikuwa wameidhinisha hatua ya kumvua uongozi wa chama hicho na kumpatia saa 24 ajiuzulu la sivyo wamuondoe madarakani. Jeshi lilichukua udhibiti wa serikali wiki iliyopita, huku mzozo kuhusu nani atamrithi ukizidi kutokota. Bw Mugabe ameonekana kupoteza udhibiti wa chama chake. Mzozo wa sasa ulianza Bw Mugabe alipomfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita, hatua iliyolikera jeshi ambalo lilitazama hatua hiyo kama jaribio la kumteua mke wake Grace kuwa makamu wa rais na mwisho kuwa mrithi wake. Haki miliki ya picha AFP/GETTY Mapema Jumapili, ...