Posts
Showing posts from October 19, 2017
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA ZANZIBAR
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku saba visiwani Zanzibar. Katika siku ya kwanza Mhe. Makamba amepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubaini fursa na changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kupata ufumbuzi. Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na masuala ya kodi, namna ya kunufaika kutoka na fursa zilizopo baina ya pande zote mbili za Muungano na kuondoa vikwazo vinavyotokana na changamoto hizo ili kuleta ufanisi. Mhe. Makamba amewahakikishia wana juimuiya hao kuwa Ofisi yake itaratibu vikao kati ya Ofisi yake na wafanyabiashara hao ili kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mambo waliyokubaliana. Mbali ya kukutana na wafanyabiashara hao Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Vyombo mbalimbali vya Habari hapa Unguja kutoa ufafanuzi wa ma...
Madiwani Waliojiuzulu Chadema Waangukia Pua Kura za Maoni CCM
- Get link
- X
- Other Apps
MADIWANI watatu wa Chadema waliojiuzulu katika Halmashauri ya Meru mkoani Arusha na kujiunga na CCM, wameangushwa katika kura ya maoni ndani ya chama hicho. Madiwani hao waliojiuzulu hivi karibuni kwa kile walichoeleza ni kutokana na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli waliomba kutetea nafasi zao. Waliogombea na kuangushwa ni Solomon Laizer, aliyekuwa diwani wa Ngabobo, Japhet Jackson (Embuleni) na Anderson Sikawa (Leguruki). Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meru, Andrew Mungure amesema leo Jumatano Oktoba 18 kuwa, matokeo ya kura ya maoni si mwisho wa uteuzi. Uchaguzi huo ulifanyika juzi Jumanne. Mungure amesema wagombea katika kata hizo watajulikana baada ya vikao ambavyo vimeanza leo. “Leo wanajadiliwa wagombea wote ngazi ya kata, baadaye tutajadili kamati ya siasa na halmashauri kuu ya mkoa ndipo watapitishwa wagombea,” amesema. Amesema kutokana na mchakato huo, matokeo ya kura ya maoni si mwisho. Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Aloyce Hayuma amekiri madiwani hao kugo...
Sharapova atupwa nje michuano ya Kremlin
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Maria Sharapova anasema muda si mrefu atarejea katika makali yake ya zamani Maria Sharapova ametupwa nje ya michuano ya kombe la Kremlin katika hatua ya kwanza siku mbili baada ya kushinda kikombe ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 2015. Sharapova raia wa Urusi mwenye miaka 30 amepoteza kwa seti 7-6 (7-3) 6-4 mbele ya Magdalena Rybarikova wa Slovakia ikiwa ni mchezo wake wa tano ndani ya siku saba. Ilikuwa pia ni mchezo wa kwanza kwa Sharapova mjini Moscow ndani ya kipindi cha miaka 10. Ushindi wake katika michuano ya China ulikuwa wa kwanza kwa kipindi cha miezi 15 alipokuwa akitumikia adhabu ya kukaa nje ya mchezo huo kutokana na kutumia dawa zilizokataliwa michezoni. Sharapova anayeshikilia nafasi ya 57 duniani alipewa kadi maalumu ya mualiko wa kushiriki michuano ya Kremlin ikiwa ni michuano ya nane kushiriki tokea alipomaliza adhabu yake mwezi April.
Manchester United yailaza Benfica ugenini
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha REX FEATURES Image caption Kipa Mile Svilar alidondokwa na machozi baada ya kufungwa bao hilo na ikamlazimu M'belgiji mwenzake Lukaku kumnyamazisha Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa sio uhalifu ''kuweka basi'' nyuma huku kikosi chake kikiishinda Benfica katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya. Bao la pekee mjini Lisbon lilifungwa na Marcus Rashford aliyepiga mkwaju wa adhabu na kumwacha kipa wa Benfica Mile Svilar bila jibu. Svila ambye ni raia wa Ubelgiji na kipa mwenye umri mdogo zaidi aliupangua mpira huo katika goli lake. Hatahivyo Rashford alikitia wasiwasi kikosi cha United baada ya kutoka nje akiguchia katika kipindi cha pili na mahala pake pakachukuliwa na Anthony Martial. United walikosolewa kwa mchezo wao katika sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi ambapo walifanya shambulio moja pekee , lakini sasa The Red Devils wamefungwa mabao sita msimuu huu.
Eden Hazard ainusuru Chelsea katika sare ya 3-3 dhidi ya Roma
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Eden Hazard akifunga mojawapo ya mabao yake mawaili dhidi ya AS Roma Eden Hazard aliwaokoa Chelsea's kuendeleza msururu wao wa kutofungwa katika kombe la vilabu bingwa baada ya Roma waliotawala mechi hiyo kutoka nyuma na kuongoza katika kiputi kilichojaa mbwembwe za kila aina katika uwanja wa Stamford Bridge. Hazard alifunga bao kila kipindi cha mchezo ,mwanzo akifunga kichwa kilichosawazisha matokeo kufuatia krosi ya Pedro zikiwa zimesalia dakika 15 mechi kukamilika katika kundi C. Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alikuwa ameipatia Chelsea uongozi wa mabao mawili katika kipindi cha kwanza baada ya David Luiz kuiweka Chelsea kifua mbele. Lakini timu hiyo ya ligi ya Serie A iling'ang'ana huku Aleksandar Kolarov akifunga kabla ya Edin Dzeko kufunga mabao mawili katika dakika sita. Shambulizi lake la kwanza ulikuwa mpira uliompita kwa juu kipa huku la pili likiwa mchezo mzuri wa nipa ni kupe kati ya Kolarov.
Conte amtaka Mourinho kuwacha kuzungumzia Chelsea
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Conte amtaka Mourinho kuwacha kuzungumzia Chelsea Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa mkufunzi mwenza katika klabu ya Manchester United Jose Mourinho anafaa kujitazama badala ya kuijadili Chelsea Conte ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu kikosi chake cha Chelsea kufuatia misururu ya majeraha msimu huu na kusema kuwa sare ya 3-3 dhidi ya Roma katika michuano ya vilabu bingwa imekifanya kikosi chake kuwa katika hali ya dharura. Mourinho ambaye amewahi kuifunza Chelsea mara mbili alinukuliwa akisema kuwa kuna wakufunzi wengine ambao hupenda kulalama sana kuhusu majeraha. ''Kila wakati Mourinho lazima azungumzie kile kinachoendelea Chelsea," alisema Conte Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Mourinho ambayo hayakumlenga Conte moja kwa moja , kocha huyo wa Itali aliongezea: Kila mara , pia msimu uliopita, nadhani ni wakati anafaa kuzungumzia kuhusu kikosi chake na ajitazame badala ya kutazama wenzake.
Viongozi 12 kukutana ili kujadili migogoro inayoendelea Afrika
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Viongozi wa bara la Afrika katika mkutano wa awali nchini Ethiopia Viongozi kutoka mataifa 12 ya bara Afrika wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Congo Brazzaville kwa mkutano wa siku mbili utakaoangazia maswala tata yanayoligubika bara hili. Mkutano huo wa kimataifa katika eneo la maziwa makuu utazungumzia migogoro kadhaa ikiwemo ile katika taifa la jamhuri ya Afrika ya kati ,Sudan Kusini, Burundi na jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC . Muhariri wa BBC barani Afrika anasema kiwango kikubwa cha fedha , rasli mali na wataalam zimetumiwa bila mafanikio katika kutataua mizozo hapo awali. Viongozi hao wa kisiasa kutoka Angola Burundi Jamhuri ya Afrika ya kati CAR ,Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo DRC , Kenya , Rwanda, Sudan , Sudan Kusini , Tanzania, Uganda na Zambia hawajakutana katika mkutano wa kiwango kama hicho tangu mwezi Juni 2016.
Mamake mwanajeshi wa Marekani asema Trump hakuwa na huruma
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha CBS Image caption Mjane wa mwanajeshi aliyeuawa akibubujikwa na machozi katika jeneza la mumewe Rais wa Marekani Donald Trump amejipata mashakani kwa mara nyingine kuhusiana na kauli yake aliyoitoa kwa mjane wa mwanajeshi wa nchi hiyo aliyeuawa vitani nchini Niger. Rais Trump amekana tuhuma kuwa alimwambia mjane wa mwanajeshi huyo kuwa mumewe alikuwa anajua kile alichoweka saini kwa kazi anayoijua hatma yake. Mamake mwanajeshi huyo ambaye aliuawa wakati wa vita ameunga mkono madai ya bunge la Congress kwamba rais Trump hakuwa na huruma wakati wa mawasiliano ya simu na mkewe mwanawe marehemu. Mbunge Federica Wilson alisema kuwa alimwambia Myeshia Johnson : Alijua alichokuwa ametia saini , ''lakini nadhani ni uchungu bila shaka''. Bwana Trump anasema kuwa madai hayo yalitungwa. Sajenti La David Johnson aliuawa nchini Niger na wapiganaji wa kiislamu mwezi huu. Alikuwa mmoja wa wanajeshi maalum waliouawa baada ya kuvamiwa. Bwana Tru...