Jeshi la Zimbabwe limekanusha madai kwamba mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kuiondoa serekali, na kudai kwamba rais Robert Mugabe na familia yake wapo salama. Katika taarifa iliyotolewa na jeshi kupitia televisheni ya taifa, imeelezwa kwamba jeshi linalenga wahalifu wanaosababisha shida za kijamii na kiuchumi na kuwafikisha mbele ya sheria. Taarifa hiyo imetolewa baada ya mashuhuda kusema wamesikia takriban milipuko mitatu pamoja na milio ya risasi katika mji mkuu wa Harare, usiku wa kuamkia Jumatano. Inaelezwa pia na mashuhuda magari ya jeshi na wanajeshi walikuwa katika mitaa mapema Jumatano hii saa kadhaa baada ya wanajeshi kushikilia chombo cha utangazaji cha serekali cha ZBC. Wakazi wamesema kwamba tofauti na kuwepo kwa taarifa ya habari ya saa tano usiku, ZBC ilicheza muziki bila taarifa yoyote. Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Harare, ameiambia VOA kwamba mitaa ya Harare ilionekana kuwa tulivu usiku wa kuamkia leo, na hakuthibitisha kuona ...