Ni nini kinachofanyika ubongoni mwa mtu akipiga miayo.
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Kupiga Miayo Unaweza kuwa unapiga miayo hivi sasa wakati ukisoma taarifa hii - ni wa kuambukiza. Sasa watafiti wamekuwa wakichunguza kinachofanyika ubongoni ili kuchochea hali hiyo. Timu ya watafiti katika Chuo kikuu cha Nottingham, imegundua kinachofanyika kwenye sehemu ya mwendo ndani ya ubongo wa binadamu. Sehemu ya primary motor cortex pia inatumika pakubwa kwenye hali kama Tourette's syndrome, yaani kinachofanyika wakati mtu anapopatwa na ugonjwa wa neva. Kupiga miayo mara kwa mara, ni dalili ya echophenomena - yaani namna ya kuiga maneno ya mtu mwingine matendo bila ya kujua. Hali hii ya Echophenomena pia inaonekama katika Tourette's, pia katika hali ya mtu kuugua kifafa na tawahudi. Haki miliki ya picha SUPPLIED Image caption Watafiti hao walitumia kifaa hichio ambacho kinajulikana kitaalamu kama transcranial magnetic stimulation Ili kufanyia uchunguzi kile kinachofanyika ndani ya ubongo wa mtu wakati wa...