Tundu Lissu Kaachiwa Kwa Dhamana Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania , Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi. Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mh Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya thamani ya milioni kumi. Aidha, Mahakama hiyo pia imemtaka Tundu Lissu kutokuondoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama. Uamuzi huo umetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri. Upande wake Tundu Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao. Tundu Lissu alitiwa katika mikono ya dola mnamo Julai 20 siku ya Alhamsi katika uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. na siku iliyofuata jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa ...
Posts
Showing posts from July 27, 2017
FLORA Mbasha na Emmanuel Mbasha Watakiwa Kuacha Utoto...Kisa Kizima Hichi Hapa
- Get link
- X
- Other Apps
Hakuna kazi ngumu kama kutoa ushauri kwa watu wenye mgogoro unaohusisha uhusiano wa kimapenzi, kwa sababu ni lazima upande mmoja utachukia, kwani ili kitu kiwe kizuri, ni lazima uwe mkweli kwa asilimia mia moja. Ni lazima mmoja atachukia kwa sababu siku zote katika uhusiano wa kimapenzi, upande mmoja unakosea. Barua yangu ya leo inawaelekea kaka na dada yangu, Emmanuel Mbasha na aliyekuwa mkewe, Flora, siku hizi akifahamika kama Madam Flora. Dada yangu Flora, ninamkubali tangu alipoanza kufanya vyema na Wimbo wa Jipe Moyo, Majaribu na nyinginezo. Dada Flora, wewe ni mtumishi wa Mungu, kama unaamini kuwa majaribu ni kipimo kwa mtu aliyeokoka, kwa nini unashindwa kumaliza bifu lenu kimya kimya ukizingatia kila mtu kwa sasa ana maisha yake mapya? Hii ni kwa sababu ya ule unaodaiwa kuwa ujumbe wako kusambaa ambao ulimsema vibaya mumeo wa zamani, kwamba alikuwa chanzo cha kuachana kwenu. Pengine maisha ya kistaa yamewaathiri au labda huenda bado mnapendana, lakin...