Arsenal yaichapa Huddersfield Town 5-0
Image caption Arsenal kwa sasa ipo nafasi ya nne na alama 28 Arsenal imeweza kutakata vilivyo ikiwa nyumbani baada ya kuichapa Huddersfield Town 5-0 katika mchezo ambao Arsenal ilitawala kila idara. Magoli ya Arsenal yamepachikwa na Alexandre Lacazette, Olivier Giroud akiingia nyavuni mara mbili, Alexis Sánchez na Mesut Özil. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema ni faraja kupata alama tatu muhimu hususan wakati huu ambapo timu zinacheza michezo mingi. Kwa upande wa David Wagner anayekinoa kikosi cha Huddersfield ametaja matokeo hayo kuwa mabaya na kuongeza kuwa ligi ya EPL ni ngumu kwani kila timu ina uwezo wa kushinda. Kwa matokeo hayo Arsenal inapanda mpaka nafasi ya nne ikiwa na alama 28.