Image caption Korea Kaskazini walaumiwa Marekani imeilalamikia Korea Kaskazini, kwa kauli yake kuwa ina haki ya kuzitungua ndege za kivita za Marekani hata kama zipo nje ya anga la taifa hilo. Msemaji wa ikulu ya Marekani ya white house Sarah Huckabee Sanders, amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini kwamba Marekani imetangaza vita,ni ya kipuuzi. Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ni kufuatia ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter,uliokuwa ukisema utawala wa Pyongyoung hauwezi kudumu kwa muda mrefu. Akizungumza katika kituo cha mafunzo cha kimataifa mjini Washington,Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha, amesema dunia inapaswa kupatiwa nafuu na maudhi ya Korea Kaskazini. "Hakika, hii inaonyesha kuwa Korea kaskazini itaendeleza maudhi yake, na katika mazingira kama haya,sisi Korea Kusini na umoja wa mataifa tunapaswa kulishughulikia suala hili kwa umakini m...