Posts

Showing posts from June 11, 2017

Wahamiaji Haramu: Kuna siku Tanzania itatawaliwa na mgeni

Image
Baptista Marco raia wa Burundi aliyekamatwa nchini hivi karibuni akifanya kazi kama mwanasheria wa TBS kinyume cha sheria.                  Matukio ya wageni kukamatwa wakifanya kazi nchini–tena nyingine nyeti–kinyume cha sheria yanazidi kuongezeka kiasi cha kuanza kujenga shaka juu ya usalama wa taifa na wananchi kwa ujumla. Hapa lazima tujiulize tatizo liko wapi; na nini kifanyike kuondoa hatari hii ambayo inaweza kutugharimu kama taifa. Wahenga walinena: usipoziba ufa, utajenga ukuta; jambo ambalo ni gharama baada ya nyumba kubomoka.              Kuna matukio ambapo wakimbizi wa kiuchumi wa kigeni wamemeajiriwa nchini na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kustukiwa. Je vyombo vyetu wa usalama vinafanya kazi gani na kama vinafanya kazi je vinaifanya vizuri? Mtu anaajiriwa kwa ngazi ya juu. Je anapataje kazi kama hakuna rushwa? Je wako wangapi wahalifu wa namna hii? Je wako peke yao au wan...

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Image
MKATABA wa kipa wa Azam FC, Aishi Salum Manula kusaini Simba umevuja kwenye mitandao ya kijamii na unaonyesha mlinda mlango huyo amesaini kwa dau la Sh. Milioni 50 kwa miaka miwili na atakuwa analipwa Milioni 3 kwa mwezi mshahara. Hata hivyo, mkataba huo unasema, Aishi atalipwa kwa awamu fedha hizo, Sh. Milioni 25 wakati wa kusiani, Milioni 5 kabla ya Agosti 30 na Sh. Milioni 20 atamaliziwa kabla ya Desemba mwaka huu. Aishi anakuwa mchezaji wa pili tegemeo wa Azam FC kuhamia Simba SC, baada ya aliyekuwa Nahodha wa timu hiyo ya Chamazi, John Raphael Bocco kutangulia pia Msimbazi kwa dau la Sh. Milioni 50 miaka miwili na mshahara wa Sh. Milioni 4 kwa mwezi. Wachezaji wote wanaondoka Azam FC wakati mikataba yao inamalizika mwishoni mwa mwezi huu na mazungumzo ya kusaini mikataba mipya yalishindikana, kutokana na sera mpya za timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kutotumia fedha nyingi katika kusajili. Aishi aliyesimama langoni jana katik...

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Image
 Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, (wa pili kulia) akikabidhi Kombe la SportPesa Super Cup kwa Nahodha wa Gor Mahia, Shakava Haron, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Leopards katika mchezo wa fainali uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.  Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar Timu ya Gor Mahia ya Kenya imetwaa ubingwa wa kwanza wa mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwasambaratisha wapinzani wao, AFC Leopards kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Uhuru.  Uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.  Kwa ushindi huo, Gor Mahia imepata nafasi ya kupambana na timu maarufu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Everton FC  Julai 13 kwenye uwanja wa Taifa jijini. Mshambuliaji wa Gor Mahia na mfungaji wa bao la kwanza kati ya matatu, Muguna Kenneth, akimtoka beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo wa Fainali...

Waziri Junior baada ya kusaini Azam ameweka wazi kile kilichomkimbiza Yanga

Image
Waziri Junior baada ya kusaini Azam ameweka wazi kile kilichomkimbiza kuingia mkataba na mabingwa wa soka nchini Yanga na kutua Azam ambapo ametamka kwamba hawakuwa siriazi na maneno yalikuwa mengi kuliko vitendo ambavyo haviendani na hali halisi. Waziri ambaye ametokea Toto African ya jijini Mwanza iliyoshuka daraja alisaini mkataba wa miaka miwili na Azam FC akitokea kuwasikiliza Yanga ambao alishawahakikishia kwamba wasiwe na wasiwasi. “Yanga walikuwa wa kwanza kuzungumza nami, Azam wamefuata, nilikwenda pale Yanga kuzungumza nao lakini wanaonekana ni watu wenye maneno mengi, sielewi tatizo ni nini ndiyo maana niliona ni vyema niende Azam ambako pia walikuwa wanahitaji huduma yangu. “Ni kweli Yanga wanashiriki mashindano makubwa lakini ushiriki wao kwangu haunisaidii kitu chochote naangalia maisha, kama kushiriki michuano mikubwa sioni maana kwani wanaenda na wanarudi bila faida, hivyo nimefanya uamuzi sahihi ambao nimeuamua mwenyewe bila kushinikizwa na mtu,” ...