Bodi ya wadhamini,TFF wakutana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mhe. Mohammed Abdulaziz (wa tatu kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wenzake na viongozi wa TFF mara baada ya chakula cha mchana na wachezaji wa Taifa Starts kwenye Hoteli ya Sea Scape, Kunduchi, Dar es Salaam Septemba 2, 2017. Wengine mstari wa mbele kutoka kushoto ni Ofisi Meneja wa TFF, Bi. Miriam Zayumba, Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Kidao Wilfred, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Abdallah Bulembo; Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Stephen Mashishanga; Rais wa TFF, Bw. Wallace Karia; Makamu Rais wa TFF, Bw. Michael Wambura na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Balozi Dk. Ramadhani Dau. Taifa Stars baadaye Jumamosi ilicheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa na kushinda mabao 2-0. (Picha na TFF). Bodi ya Wadhamini wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana na viongozi wakuu wa Shirikisho katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Sea Scape, Kunduchi, Dar es...