Posts

Showing posts from November 29, 2017

Tyson Fury: Nitataka kupigana na mtu mwenye jina kubwa zaidi

Image
Image caption Fury baada ya kumchapa Wladimir Klitschko mwaka 2015 Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury amesema atapenda kupigana na mtu mwenye jina kubwa iwapo atarejea uwajani. Fury mwenye miaka 29 tiyari ameshasaini mkataba na kampuni ya MTK akijiandaa kumaliza adhabu yake. Anatarajia kusikia uamuzi wa mahakama mwezi Desemba dhidi ya kesi yake ya matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni mwaka 2016. ''Naweza kuitwa mkorofi, mgomvi na mambo mengine ya aina hiyo, lakini sio mtumizi wa dawa za kuongeza nguvu,'' alisema Fury raia wa Uingereza. Chama cha ndondi nchini Uingereza kimesema bingwa huyo ambaye alipata mikanda ya IBF, WBA na WBO kwa kumchapa Wladimir Klitschko Novemba 2015, hatopewa leseni ya kupigana mpaka pale mambo yote yatakapowekwa sawa.

Manchester United yaichapa Watford 4-2

Image
Image caption Ashley Young alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo Manchester United ikiwa ugenini katika dimba la Vicarage Road imefanikiwa kuichapa Watford 4-2 katika ushindi ambao awali ulionekana kuwa mgumu kwa United kabla ya kuanza kwa mchezo. Magoli ya United yamefungwa na Ashley Young akiingia nyavuni mara mbili huku Antony Martial akipachika goli la tatu na Jesse Lingard. Troy Deeney na Doucaure walindika magoli mawili ya Watford. Meneja wa Manchester United José Mourinho amesema ushindi huo utaongezaotisha kwa timu yake. Image caption Wachezaji wa Watford wakishangilia Man United inasalia nafasi ya pili ikiwa na alama 32 ikiwa ni alama tano nyuma ya Man City ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi.

Uchaguzi Kenya: Kenyatta aapishwa na kuahidi kuliunganisha taifa

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Kenyatta ameapishwa kuongoza kwa muhula wa pili na wa mwisho Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameahidi kuunganisha taifa hilo katika muhula wake wa pili uongozini baada ya kuapishwa katika sherehe ambayo ilisusiwa na viongozi wa upinzani. Akihutubu baada ya kula kiapo uwanjani Kasarani, Nairobi kiongozi huyo alisema ameyasikia baadhi ya mapendekezo ya upinzani na atazingatia baadhi. Hata hivyo aliwahimiza viongozi wa upinzani kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo. Muungano wa upinzani, ambao ulisusia uchaguzi wa marudio tarehe 26 Oktoba, ulikuwa umepanga mkutano wa hadhara kuombolewa wafuasi wa muungano huo ambao wameuawa katika makabiliano na maafisa wa polisi. Mkutano huo haukufanyika kama ulivyopangwa katika uwanja wa Jacaranda, lakini kiongozi wa National Super Alliance Raila Odinga akihutubia wafuasi wake karibu na uwanja huo alitangaza mpango wa kumuapisha kuwa rais mwezi ujao tarehe 12, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Jamhur...

Korea Kaskazini yarusha kombora 'lililoruka juu zaidi'

Image
Image caption Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa kombora hilo linaweza kufika mahala popote pale duniani Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis. Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka katika maji ya Japan. Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini. Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya wasiwasi. Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba. Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo. Image caption Gwaride la kijeshi la taifa la Korea Kaskazini Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa....

Mwanamfalme Miteb aachiliwa huru baada ya kulipa $1bn Saudia

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mwanamfalme Miteb aachiliwa huru baada ya kulipa $1bn Saudia Mwanamfalme wa Saudia Miteb bin Abdullah ameachiliwa huru zaidi ya wiki tatu baada ya kukamatwa kwa madai ya kuhusika na ufisadi , maafisa wanasema. Mwanamfalme Miteb ambaye alionekana kuwa miongoni mwa warithi wa ufalme huo aliachiliwa huru baada ya kukubali kutoa faini ya dola bilioni moja. Ni miongoni mwa wanasiaasa na wafanyibiashara 200 waliokamatwa nchini humo kutokana na vita dhidi ya ufisadi mnamo terehe 4 mwezi Novemba. Watu wengine watatu pia wameachiliwa huru baada ya kukubali kulipa faini. Ni kweli mwanamfalme Miteb aliachiliwa huru leo alfajiri {Jumanne} kulingana na duru zilizopo karibu na serikali zilizoambia chombo cha habari cha AFP. Miteb ambaye ni binamu wa mwanamfalme Mohammed bin Salman na ambaye aliongoza kitengo cha walinzi wa kulinda ufalme huo ndiye aliyekuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa kisiasa kukamatwa katika vita hivyo dhidi ya ufisad...

Korea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kombora hilo lililorushwa nyakati za giza alfajiri siku ya Jumatano lina uwezo mkubwa kushinda kombora lolote lile a taifa hilo Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo lolote la Marekani. Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia. Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano. Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo . Kitengo cha habari cha taifa hilo KCNA kilisema kuwa kombora hilo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53. Kombora hilo lililofyatuliwa kwa mwinuko halikupitia katika anga ya Japan kama makombora mengine hapo awali na lilianguka kilomita 250 karibu ...