Chid Benz awekwa chini ya uangalizi na mahakama kwa kutumia dawa za kulevya
Chid Benz awekwa chini ya uangalizi na mahakama kwa kutumia dawa za kulevya . Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chid Benzi (pichani) na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo dhidi ya maombi hayo. Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za kulevya. Maombi hayo yalisikilizwa na kutolewa uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Ritha Tarimo. Mbali na Chidi Benzi, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed. Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha hati ya kiapo kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama itoe dhamana kwani w...