Tamko la Serikali kuhusu homa ya Ini,
Serikali imesema kuwa inatarajia kuanza kutoa Chanjo ya Homa ya Ini kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha kwa wale wote wenye dalili za ugonjwa au wenye ugonjwa wa Ini. Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani. “Katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo, watapata chanjo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti 2018/2019” alisema Ummy. Alisema kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu. Aidha, Ummy alisema kuwa asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga s...