Posts

Showing posts from September 19, 2017

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 19, 2017- NDANI NA NJE YA TANZANIA

Image
Magazetini leo Jumanne September 19, 2017

Rais Trump Anasema Taasisi ya Umoja Wa Mataifa Haifanyi Vizuri

Image
Rais Donald Trump akiwa na balozi Nikki Hailey Rais wa Marekani Donald Trump alifungua mzunguko wa majadiliano ya pamoja Jumatatu mwanzoni mwa vikao vya kidiplomasia vya siku nne huko New York nchini Marekani kwa ajili ya kikao cha mwaka cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa na mikutano mingine ya pembeni.  Akionekana kwa mara ya kwanza kwenye Umoja wa Mataifa hiyo Jumatatu siku moja kabla ya kufunguliwa rasmi kwa kikao cha baraza kuu Rais Trump aliongoza kikao kuhusu mageuzi katika taasisi hiyo ya dunia na kutaka hatua za kijasiri zichukuliwe kuifanya taasisi hiyo yenye mataifa wanachama 193 iwe taasisi yenye nguvu kwa amani. Rais Trump (C) na wanadiplomasia katika UN Akizungumza pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na balozi wa Washington katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, Rais Trump aliwaambia wanadiplomasia kwenye mkutano wa mageuzi kwamba taasisi hiyo haifanyi vizuri kama inavyotakiwa na kwamba uras...

Saa 72 ngumu kwa Yusuf Manji

Image
Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yusuf Manji atakuwa na wakati mgumu angalau kwa saa 72 atakapotoa utetezi dhidi ya kesi inayomkabili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin. Kesi hiyo ambayo ipo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha itasikilizwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatatu ijayo. Ushahidi wa upande wa utetezi ulikuwa uendelee jana, lakini kutokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani upande wa utetezi uliomba muda hadi Jumatatu kuendelea na ushahidi. Manji anatarajia kuwaita mashahidi 15, huku mmoja ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akiwa ameshatoa ushahidi wake. Pia, upande wa mashtaka walidai wangewaita mashahidi wasiozidi 10, lakini walifika watatu. Awali Hakimu Mkeha alimuuliza Manji sababu za kuchelewa mahakamani wakati ilipaswa kuanza saa tatu asubuhi. Kutokana na swali hilo, Manji aliomba msamaha kwa kuchelewa kwa madai alipitia hospitali na kwamba alikuwa amemueleza waki...

ZAIDI YA WAKAZI 5,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA USAMBAZAJI MAJISAFI KIMARA KILUNGULE B JIJINI DAR

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akizungumza wakati wa uzindulizi mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka na Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota.   Diwani wa Kimara, Paschal Manota akizungumza wakati wa uzindulizi mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka na Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota. Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo ambao umezinduliwa leo eneo la Kilungule B, ambapo walikuwa hawakuwahi kuipata huduma hiyo kwa miaka 20. Aliongeza ku...