Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.12.2017
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Luke Shaw Mlinzi wa Manchester United Luke Shaw anahitaji pauni milioni 5 kulipa ili kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari. NewCastle walikuwa wanamtaka mchezaji huyo wa miak 22 lakini hawakuwa wanataka kulipa pauni millioni 20 ambazo United walikuwa wanahitaji. (Sun) United pia wamefanya mazungumzo na mchezaji wa safu ya kati Marouane Fellaini katika jaribio la kutaka asaini mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa Felliani unakamilika msimu huu. (Sun) Gareth Bale amakubalia na na Real Madrid kuondoka klabu hiyo msimu ujao, huku Manchester United na Tottenham wakimwinda mshambuliaji huyo wa miaka 28 (Diario Gol) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Gareth Bale Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji Olivier Giroud, 31, atasalia klabu hiyo. Giroud amekuwa anataka kuoondoka klabu hiyo kwa mkopo. (Daily Mirror) Juventus wanatathmini kumsaini mlinzi wa Arsenal, Hector Bellerin, 22. (Sun kupitia Tuttosp...