Utata umegubika mradi wa ujenzi wa mji wa Kisasa Kigamboni jijini Dar es Salaam uliokuwa ukitekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Azimio Housing Estates baada ya kuibuka taarifa za kuuzwa. Taarifa za kuuzwa kwa mradi huo ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii na hazikukanushwa na NSSF wala Serikali. Lakini alipoulizwa jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Profesa Samuel Wangwe alikanusha kuuzwa kwa mradi huo akisema wanataka kuingia ubia na kampuni nyingine ili wauendeleze. “Ule mradi tunajaribu ‘kuu-scale down’ (kurahisisha) na kufanya uwe ‘profitable’ (faida), siyo kuuza ila kutafuta ‘partner’ (mbia) ili achukue ule mradi. Kwa hiyo ni ‘joint venture’ (ubia). Bado hatujapata, ‘tuna-negotiate’ (tunajadiliana),” alisema Profesa Wangwe. Licha ya NSSF kukanusha kuuza mradi huo maarufu kwa jina la Dege Eco Village, kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart imesema kuna mchakato unaendelea na taarifa ...