Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 20.11.2017
Image caption Mshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24, Manchester City itashindana na Liverpool kumununua beki wa Southampton na Uholanzi Virgil van Dijk, 26, katika dirisha la uhamisho la Januari.{Daily Mirror}. City pia inataka kumsajili kiungo wa kati wa Schalke na Ujerumani Leon Goretzka ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu na amewavutia Arsenal, Liverpool na Chelsea (Daily Mirror) Mshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24, anasema kuwa anapanga kuichezea Tottenham kwa kipindi chote cha mchezo wake kilichosalia (London Evening Standard) Image caption Daniel Sturridge Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 28, yuko tayari kuondoka Liverpool ili kuweza kuchezeshwa na kuweza kuhifadhi nafasi yake katika timu ya Uingereza. (Daily Mirror) Barcelona inapanga kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil na inaweza kumuuza mchezaji wa Ureno Andre Gomes badala yake (Don Balon - in Spanish) Nahodha wa Paris S...