Posts

Showing posts from July 25, 2017

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

 Ili iitwe sabuni inatakiwa -Ngumu kuiisha -Yenye povu jingi -Nyeupe VIAMBATA VYA kutengenezea sabuni Mafuta-mawese,mise,wanyana Maji Caustic soda(costiki soda) VIFAA VYA KUTENGENEZEA Ndoo za plastiki lita 20 nne Diaba 1 Mti wa kukorogea Mashine ya kukorogea Box la kugandishia Mhuri wa biashara Mzani wa saa Vibao vya kukatia VIFAA VYA USALAMA Mask Groves Gum boots Goggles (miwani) Overall Ndoo ya maji au mchanga FORMULA mafuta lt1+caustic soda grm135+maji mls350+sodium siligate prm100. KUCHANGANYA pima maji ktk ndoo ya plastic kisa weka caustic soda ktk maji weka kidogokidogo huku ukikoroga mpaka itakapo yeyuka.mchanganyiko huu unaweza kuchemka na kutoa mosh usiogope. acha ipoe kuanzia masaa 8 nazaidi. KUCHANGANYA NA MAFUTA yeyusha mafuta kwa kuyapasha joto kidogo ambapo unaweza kuyashika, tia sangi na mimina kidogo2 kuchanganya michanganyiko huku ukikoroga. mimina kwenye box la kugandishia acha igande tayari kwa kukata.Pia weka sodium siligate

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Image
Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mba...

UTENGEZAJI WA JUIS MBALIMBALI

Image
                                                   JUISI YA UKWAJU   Huhitaji kutumia gharama kubwa na ni rahisi kutengeneza juisi hii ya ukwaju. Mahitaji: -Maji ya moto lita moja -Ukwaju wa kutosha -Jagi au birika lenye uwezo wa kutosha maji lita moja au zaidi Jinsi ya kutengeneza: Weka maji yako ya moto kwenye jagi au birika lako kisha weka ukwaju ndani yake (ukwaju uliotolewa maganda). Acha ukwaju ndani ya maji ya moto kwa muda hadi maji yatakapopoa kabisa. Baada ya hapo koroga mchanganyiko huo hadi uhakikishe kuwa juisi imekuwa nzito. Kisha mimina juisi yako kwenye jagi lingine kuchuja mabaki ya ukwaju (usichuje juisi kwa chujio la chai). Baada ya hapo juisi yako itakuwa tayari kutumika. Lakini usiweke sukari wala kitu kingine choc...

JAFO AINYOOSHEA KIDOLE OFISI YA MGANGA MKUU MKOA WA KAGERA

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa wakiangalia baadhi ya miundombinu ya Zahanati ya Ihembe 2 yanayoanza kuharibika kutokana na kutotumika. Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika ukaguzi wa Zahanati ya Ihembe 2 wilayani Karagwe. Nyumba ya Mganga wa Zahanati ya Ihembe 2 iliyotelekezwa licha ya kukamilika. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo akiwa katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera amekerwa na tabia ya baadhi watendaji kwa kutoguswa na matatizo ya wananchi na kuendekeza kukaa ofisini. Akiwa wilayani humo leo, Jafo amesema watendaji hao wamekuwa wakikaa ofisini bila ya kufika maeneo ya wananchi na kubaini juhudi kubwa zinazofanywa na jamii na kwa upande wao kama wataalam waweze kufanya majukumu yao kwa lengo la kuwapatia wananchi huduma.   Naibu Waziri Jafo...

MSANII LINAH AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

Image
MSANII LINAH AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE Linah . Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama Linah amejifungua mtoto wa kike salama katika hospitali ya Marie Stopes, Mwenge jijini Dar es Salaam. Linah amejifungua leo, Jumanne, Julai 25 ikiwa ni muda mfupi baada ya maneno ya mashabiki zake kusambaa kwamba ujauzito wake ni wa muda mrefu tofauti na ilivyo kawaida. Alipokuwa mjamzito. Mtu wa karibu na msanii huyo amesema kuwa mama na mtoto kiafya wanaendelea vizuri. Hata hivyo katika kipindi chote cha ujauzito wake, Linah amekuwa akimtaja mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina moja la  Shaban  kwamba ndiye baba wa mtoto wake. Miaka kadhaa nyuma, Linah amewahi kuzungumzia kuhusu taarifa za kuharibika kwa ujauzito wake wa kwanza ambao ulikuwa wa mpenzi wake wa zamani