Said Alf awakimbia CHADEMA, Ataka ubunge kwa CCM sos.Mpekuzi blog MBUNGE wa Jimbo la Mpanda Mjini, Bw. Said Amour Alfi (CHADEMA) ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wamechukua na kurejesha fomu za kuomba kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Nsimbo, Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa CCM mkoani Katavi, Averin Mushi amethibitisha Bw. Arfi kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo hilo. Alisema makada 23 wamejitokeza kuwania ubunge katika majimbo yote ya uchaguzi mkoani humo ambapo katika Jimbo la Nsimbo, makada ambao wamerejesha fomu ni Bw. Arfi, Shabir Hasanali 'Dallah', Richard Mbogo, Manamba David na Mapesa Frank. Katika Jimbo la Katavi ni Isaack Kamwelwe, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo, Shafi Mpenda, Maganga Kampala na Osca Albano. Kwa upande wa Jimbo jipya la Kavuu, yupo Zumb...