Posts

Showing posts from September 28, 2017

MAGAZETI YA TZ NA NJE SEPT 28,2017

Image

Lema, Nassari wafurahia kupeleka ushahidi Takukuru

Image
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema wamefurahia kauli ya mkurugenzi mkuu wa Takukuru kuwataka kupeleka ushahidi wa tuhuma zao kuwa kulikuwa na mchezo mchafu kushawishi madiwani wao kujiunga na CCM mbele ya Rais John Magufuli katika hafla ya kiserikali iliyofanyika jijini Arusha wiki iliyopita. Lema na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari walidai kuwa madiwani wawili wa Chadema waliotangaza kujiunga na CCM wakati wa hafla ya kukabidhi kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, walishawishiwa kwa rushwa na kwamba kitendo hicho kilifanyika katika ofisi za Serikali na wanao ushahidi usio na shaka. Diwani mpya aliyeihama Chadema na kujiunga na CCM ni Rayson Ngowi wa Kata ya Kimandolu ambaye hata hivyo alikana kurubuniwa kufikia uamuzi huo. Walimuomba Rais Magufuli awaite ili wampatie ushahidi huo kuonyesha kuwa kitendo hicho ni kinyume na juhudi zake za kupambana na rushwa. Jana, Lema aliiambia Mwananc...

MARUFUKU SHULE MKOANI SINGIDA KUNUNUA CHAKI NJE YA MKOA-RC NCHIMBI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa. Dkt Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na ikiwa haijapata soko. “Hawa wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza kuwa, “Yani mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”. Dkt Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa kuunga mkono viwanda hivyo. Am...

Kyle Edmund achapwa na Dolnadson -Michuano ya Chengdu

Image
Image caption Kyle Edmund Michuano ya Chengdu, China, Kyle Edmund ameshindwa kutamba katika michuano hiyo baada ya kufungwa na mpinzani wake Jared Donaldson katika raundi ya pili ya mchezo kwa seti 6-0, 1-6, 6-4 . Awali Edmund alimfunga Bernard Tomic katika mzunguko wa kwanza kabla ya kuvaana na Donaldson. Michuano hii ya Chengdu inaendelea tena hii leo kwa michezo mbalimbali, Andrey Rublev anacheza na Yen-Hsun Lu, Marcos Baghdatis dhidi ya Peter Gojowczyk, Taylor Fritz na Nikoloz Basilashvili, Dominic Thiem anachuana na Guido Pella,Santiago Gonzalez dhidi ya Nenad Zimonjic,Treat Huey acheza na Fabrice Marti na Julio Peralta dhidi ya Michael Venus. Marcus Daniell anamkabili Marcelo Demoliner, Jonathan Erlichdhidi ya Aisam-Ul-Haq Qureshina Leonardo Mayer atachuana na Albert Ramos, Yen-Hsun Lu anachuana na Divij Sharan, Dominic Inglot atakimbizana na Daniel Nestor.

Hasheem Thabit kujiunga na Yokohama

Image
Haki miliki ya picha GOOGLE Image caption Mchezaji wa zamani wa Timu ya OKC Thunder ya ligi kuu ya Marekani (NBA) Mtanzania Hasheem Thabi Mchezaji wa zamani wa Timu ya OKC Thunder ya ligi kuu ya Marekani (NBA) Mtanzania Hasheem Thabit kwa sasa amejiunga na Timu ya Yokohama B Corsairs ya Ligi kuu ya kikapu ya Japan, kwa dau ambalo mpaka sasa halijawekwa wazi, na tayari Thabit amekabidhiwa Jezi yenye namba 34 katika timu hiyo.  Ligi ya kikapu ya Japan B-League inatarajiwa kuanza kesho ijumaa wiki hii, na Hashee yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili.

Basel yaichapa Benfica 5-0 Uefa

Image
Image caption Basel yaichapa Benfica 5-0 Michuano ya kuwania taji la Klabu Bingwa Barani Ulaya (Uefa champions Ligi) imechezwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi katika hatua ya makundi kwa michezo mbalimbali. Kundi A- FC Basel wakiwa nyumbani wameibugiza Benfica 5-0, CSKA Moscow wakiwa nyumbani walikubali kipigo cha mabao 4 -1 na Manchester United huku Romelu Lukaku akifunga mara mbili, Martial na Mkhtaryan walifunga bao moja moja huku bao la Moscow likifungwa na Kuachev na kuwafanya United kuongoza kundi A. Kundi B - Psg wakiwa nyumbani wameshinda mabao 3-0 dhidi ya Buyen Munich ambapo wachezaji Dani Alves, Neyamar na Edison Cavanni wamefanikiwa kuifunga Bayern Munich bao 3 huku Celtic wakiwa ugenini wakiifunga Anderchelt mabao 3 mabao ya Celtic yakiwekwa kimiani na Patrick Roberts, Scott Sinclair na Griffiths. Kundi C FC Qarabag imechapwa 2-1 na AS Roma, Atletico Madrid imefungwa 2-1 dhidi ya Chelsea. Kundi D- Gonzalo Higuain na Mario Mandzukic waliisaidia Juventus kupata ala...