Posts

Showing posts from August 11, 2017

Vita ya Diamond Platnumz na Alikiba Kuamuliwa Nigeria

Image
Jana usiku majina ya wasanii waliochaguliwa kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za AFRIMA 2017 yametangazwa ambapo kwenye kipengele cha Msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki mahasimu Diamond Platnumz na Alikiba wamekutana tena kwenye kipengele hicho na ndiyo Wasanii pekee waliofanikiwa kuingia kwenye kipengele hicho. Wasanii wengine kutoka Tanzania waliotajwa kwenye tuzo hizo ni Lady Jaydee, Nandy na Vanessa Mdee wote wapo kwenye kipengele cha msanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki. Upigaji kura wa Tuzo hizo utaanza Tarehe 21 Agosti mwaka huu na zitatolewa tarehe 12 mwezi Novemba huko Lagos nchini Nigeria, Tazama Orodha kamili ya tuzo za AFRIMA 2017 hapa chini.

Waziri Mwijage Acharuka.......Avifunga Viwanda 10 kwa Kushndwa Kuendelezwa

Image
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amesema serikali imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya kutwaa viwanda walivyopewa wawekezaji na kushindwa kuviendeleza huku viwanda vingine vikiwa chini ya uangalizi wa muda Waziri Mwijage amesema hayo jana Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao kilichojumuisha wawakilishi wa Wizara za Fedha, Tamisemi na Wizara ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu. Amevitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha korosho Lindi, Mgodi wa Pugu Kaolin, Mkata Saw Mills Ltd, Manawa Ginnery Co Ltd, Kiwanda cha Chai Dabaga, Tembo Chipboard Ltd, Kiwanda cha Nguo cha Kilimanjaro, Mang’ula Mechanical and Machine Tools co. Ltd na Polysacks cha Dar es Salaam. Aidha, Mhe. Mwijage amesema serikali ambayo awali ilibinafsisha mashirika 341 ya umma ambayo yalijumuisha viwanda, mashamba, makampuni ya biashara, mahoteli na makampuni ya usafirishaji lakini kati ...

Tume ya uchaguzi Kenya yashangazwa na matokeo ya upinzani

Tume ya Uchaguzi ya Kenya imesema ni mapema na ni kinyume cha sheria kwa mgombea wa upinzani Raila Odinga kujitangazia kuwa ameshinda uchaguzi wa Kenya. Alhamisi, muungano wa upinzani wa NASA ulichapisha matokeo ambayo yanaonyesha kuwa Raila Odinga amemshinda Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, ambapo pia waliitaka tume ya uchaguzi imtangaze Odinga kuwa ndiye Rais mteule. Hata hivyo matokeo ya awali hadi sasa yaliyotangazwa na tume hiyo yanaonyesha Rais wa sasa Uhuru Kenyatta bado anaongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga. Mwandishi wetu Anne Soy alifanya mahojiano na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati. Kwanza alimuuliza, je tume hiyo imepokea barua yoyote kutoka upinzani?