Posts

Showing posts from August 29, 2017

Comment ya Bilionea wa 20 Afrika kwenye post ya Alikiba

Image
Staa wa Rock Star  Alikiba  ambaye anafanya vizuri kwenye game ya Bongofleva husani na video yake mpya ya  ‘Seduce Me’  kwa kuweka rekodi ya kufikisha zaidi ya views milioni mbili  YouTube  ndani ya siku tatu, anazidi kupokea pongezi kutoka kwa watu mbalimbali. Alikiba Alikib a ambaye video ya wimbo wake wa  ‘Seduce Me’  inafanya vizuri kwa sasa amepata pongezi kutoka kwa mfanyabiashara na bilionea wa 20 Afrika kwa mujibu wa mtandao wa  www.forbes.com   Mohamed Dewji   kupitia ukurasa wake wa instagram. Mohamed Dewji MO Dewji   amecomment katika post ya  Alikiba  ya kushukuru mashabiki na watu mbalimbali ambao wamesapoti video yake kufikisha views milioni mbili ndani ya siku tatu katika mtandao wa  YouTube .

Ian Wright: Wenger anafaa kuondoka Arsenal

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Ian Wright asema kuwa Wenger anafaa kuondoka Arsenal Arsenal iko katika hali mbaya ''kuanzia juu hadi chini'' na mkufunzi Arsene Wenger anafaa kuondoka kulingana na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Ian Wright. Kichapo cha 4-0 dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili kiliiwacha timu hiyo na ushindi mmoja pekee kati ya mechi zake za kwanza tatu za ligi. ''Ni ndoto mbaya'', alisema Ian Wright ambaye aliifungia Arsenal mabao 128. ''Kwa nini tusipate wachezaji wanaoweza kuichezea Arsenal'',? ''Wenger ndio wa kulaumiwa'', aliambia BBC. Wright ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha Wenger walioshinda kombe la FA mara mbili 1997-98 aliongezea: Matatizo yanamrudia mwenyewe. ''Tumecheza mechi tatu na tuko mashakani tayari.Je anafaa kwenda? ndio ningependelea aondoke kwa sababu sidhani kwamba anaweza kuwapatia motisha wachezaji''. ''Ni k...

Wakazi wa Shinyanga na Geita kunufaika na uwekezaji mradi wa umeme

Image
Kampuni ya Acacia, kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo. Acacia imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za Geita. Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Haya ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji. Mkuu wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine. “Ujenzi wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotoka...

Trump aagiza maafisa wa polisi kupewa vifaa vya kijeshi Marekani

Image
Haki miliki ya picha Image caption Mwanasheria mkuu Jeff Sessions asema ni muhimu kwa polisi kupokea vifaa ili kufanya kazi yao vyema Rais wa Marekani Donald Trump ameondoa marufuku iliowekwa na Obama kuhusu kuwapatia maafisa wa polisi vifaa vya kijeshi. Agizo hilo la rais sasa litawaruhusu maafisa wa polisi kupokea vifaa vya kijeshi ikiwemo magari ya kijeshi na kofia zisozoweza kuingia risasi. Mwanasheria mkuu Jeff Sessions amesema kuwa lengo lake kuu ilikuwa kuimarisha usalama miongoni mwa raia. Bwana Obama alilizuia jeshi kutowapatia maafisa wa polisi vifaa vyake kufuatia mgogoro wa Missouri. Marufuku hiyo ilifuatia shutuma kwamba maafisa wa polisi walikuwa wazito kupitia kiasi kukabiliana na waandamanaji kufuatia mauaji kijana mmoja mweusi yaliotekelezwa na polisi mzungu 2014. Rais huyo wa zamani alikuwa na wasiwasi kuhusu maoni ya raia kuhusu maafisa wa polisi waliovalia magwanda mazito ya kijeshi akisema kuwa ilikuwa muhimu kwamba maafisa wa polisi walifaa kuone...

Israel: Iran inajenga kiwanda cha makombora Syria

Image
Haki miliki ya pich ALAMY Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inatengeza kiwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inajenga viwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora. Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuifanya Syria kuwa kambi yake kutengeza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel. Majeshi ya Iran yanamsaidia rais Bashar al Assad katika vita vya Syria huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah. Matamshi ya Netanyahu yanajiri baada ya kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutierrez mjini Jerusalem. Bwana Guterres amefanya ziara yake ya kwanza katika enewo hilo tangu kuchukua mamlaka mnamo mwezi januari. Bwana Netanyahu hakutoa maelezo kuhusu viwanda hivyo vya Iran lakini akaonya kwamba hicho ''ni kitendo ambacho Israel haitakubali''. Wiki mbili zilizopita, k...

Korea Kaskazini yaichokoza Japan

Image
Haki miliki ya picha Image caption Kiongozi wa Korea kaskazini na makamanda wake Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini. Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido. Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara. Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake. Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini. Wanajeshi wa Marekani na Japan wanafanya zoezi la pamoja katika eneo hilo la Hokkado, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in aliagiza uwezo wa utumiaji wa nguvu ili kujibu shambulio hilo. Ndege nne za Korea Kusini zilifanya zoezi la kurusha ...