CHELSEA, ARSENAL SARE, MAN UNITED SPIDI 100
Wachezaji wa Man U wakishangilia kwa pamoja baada ya kutupia bao la tatu dhidi ya Everton. DAVID Luiz jana alipewa kadi nyekundu wakati timu yake ya Chelsea ilipotoka suluhu na Arsenal, huku Man United wakiichapa Everton bao 4-0. Katika mchezo wa kwanza, Arsenal walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, lakini wakaonyesha kiwango cha hali ya juu sana huku wakikosa nafasi kadhaa za wazi kipindi cha kwanza. Hata hivyo, timu zote mbili haziwezi kufurahia sare hiyo kutokana na upinzani mkali uliopo kwenye Ligi Kuu England kwa sasa. Wakifanya yao. Arsenal ambao waliifunga Chelsea kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA mwaka jana na kuwachapa tena kwenye Ngao ya Jamii mwanzoni mwa msimu huu, walionekana kumiliki mchezo huo kwa asilimia kubwa sana mwanzoni. Lakini Chelsea nao waliibuka kipindi cha pili na kukosa nafasi kibao. Hii ni sare ya kwanza kwa timu hizo mbili kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, baada ya kupita miaka 12. Awali, Arsenal ilikuwa ikikum...