TGNP MTANDAO YA ADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUYAFANYA HAYA...
Leo june 6 ikiwa ni siku ya Mototo wa Afrika Mtandao wa jinsia nchini Tanzania TGNP ukishirikiana na vituo vyake vya taarifa na maarifa umefanya semina iliyokutanisha wanafunzi toka shule mbalimbali za jijini Dar es salaam. Kwenye semina hiyo kulikuwa wanafunzi toka shule ya sekondari Mabibo, Kivule sekondari, shule ya msingi Mchangani na wenyeji shule ya sekondari Makumbusho. Lakini pia walikuwepo viongozi mbalimbali kama Diwani viti maalum wa kata ya Makumbusho Bi. Pilly Ochaya, Afisa ustawi wa jamii wa manispaa ya Kinondoni Bi. Editha Mbowe na viongozi wa mitaa na kata ya Makumbusho. Mkurugenzi wa (JIKI Tanzania) na Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa kata Makumbusho Bi. Janeth Mawinza akiongoza tafrija ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika shule ya Sekondary Makumbusho mapema leo jijini dar es salaam. Kwenye mkutano huo kumeibua changamoto mbalimbali zinazowakabiri wanafunzi wa shule zote za sekondari na za msingi. miongoni mwa changamoto kubwa ina...