Posts

Showing posts from August 1, 2017

MSICHANA ALIYE FALIKI PAMOJA NA CHRIS MSANDO .

Image
Picha ni Caro Ngumbu, 21, ambaye mwili wake ulikutwa pamoja na mwili wa IEBC ICT manager Chris Msando. Caro Ngumbu, 21, anatokea  Gachie, Kiambu county,na alimaliza masomo yake ya uhuguzi   Karen campus of Kenya Medical Training College.(KMTC) Chris Msando alisema mfumo wa kielectronic wa kupiga kula hauta  dukuliwa na chama chochote.

Tangazo la Uhuru kufuatia mauaji ya kinyama ya Msando lililowasha moto mitandaoni

Image
Wananchi wamekasirishwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kutoa taarifa kuhusiana na mauaji ya meneja wa habari, mawasiliano na teknolojia wa IEBC Chris Msando -Uhuru aliomboleza kifo cha Msando na kile cha Carole Ngumbu, ambaye alikuwa na meneja huyo wakati wa kifo chake Rais Uhuru Kenyatta ameshambuliwa na wananchi baada ya kuomboleza kifo cha meneja wa habari, mawasiliano na teknolojia wa IEBC Chris Msando na Carole Ngumbu, ambaye alikuwa na meneja huyo wakati wa kifo chake. Uhuru aliandika kama ifuatavyo kwenye ukurasa wake wa tweeter, Uhuru Kenyatta   ✔ @UKenyatta We are all deeply shocked and saddened by the murder of Chris Msando and Caro Ngumbu. 4:10 PM - Aug 1, 2017   421 421 Replies     217 217 Retweets     432 432 likes

Usain Bolt afananishwa na Muhammed Ali

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Usain Bolt afananishwa na aliyekuwa bingwa wa ndondi Muhammed Ali Usain Bolt ana kipaji na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama Muhammed Ali alivyokuwa na ushawishi miongoni mwa mabondia, alisema Lord Coe. BIngwa huyo wa mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini London, yalioanza siku ya Ijumaa. Coe alimfananisha raia huyo wa jamaica na mmoja wapo wa wanamichezo mashauri duniani Muhammed Ali. Ni bingwa wa mbio fupi duniani,alisema Coe ambaye ndio raisi wa shirikisho la wanariadha duniani IAAF. Usain Bolt ana kipaji.Siwezi kumfananisha na mwanamichezo mwengine yeyote yule zaidi ya Muhammad Ali, ambaye amekuwa na ushaiwishi mkubwa nje na ndani ya michezo. Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu ni nani mchezaji bora wa soka duniani ama mchezaji wa tenisi bora, lakini hakuna mjadala kuhusu Bolt katika mbio fupi. Mwanariadha...

Los Angeles kuandaa Olimpiki 2028

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Carl Lewis Jimbo la Los Angeles limeteuliwa rasmi kuandaa mashindano ya Olimpiki ya wakati wa majira ya joto mwaka 2028 katika makubaliano yatakayoihakikishia Paris kuandaa Olympiki ya mwaka 2024. Miji yote miwili ilikuwa akipigania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa duniani katika tarehe za awali. Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amesema anakaribisha uamuzi huo wa Los Angeles kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa tarehe za mbele. Kamati hiyo ya Olimpiki imesema itatoa mchango wake wenye thamani ya dola bilioni 0.8 kwa mji wa Los Angeles ili kufidia gharama zitakazoongezeka.

Man Utd wakamilisha kumnunua Nemanja Matic kutoka Chelsea

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Manchester United wamekamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kutoka kwa mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea kwa £40m. Mchezaji huyo ametia saini mkataba wa miaka mitatu. Matic, 28, amekuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na United majira haya ya joto. United walikuwa wamemnunua beki Victor Lindelof kwa £31m kutoka Benfica na kisha wakalipa £75m kumchukua Romelu Lukaku kutoka Everton. Meneja wa United Jose Mourinho alimweleza Matic kama mchezaji anayecheza vyema na wenzake kwenye timu na "ana kila kitu ambacho tungetaka katika mwanakandanda; uaminifu, uendelevu na kuwa na ndoto kuu". Matic amesema ana furaha sana kujiunga na United wakati huu wa kusisimua. Mourinho, alipokuwa Chelsea, alitumia £21m kumnunua Matic kutoka Benfica kwa kipindi cha pili Stamford Bridge Januari 2014. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Nemanja Matic aliachwa nje ya kikosi cha Chelsea kilichosafiri bara Asia kujiandaa kwa ...

Trump alimfunza mwanawe maneno ya kusema mkutanoni

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Bwana Trump Jr na wakili wa Urusi Natalia Veselnitskaya Rais Donald Trump alimfunza mwanawe maneno aliyofaa kusema kuhusu mkutano na wakili wa Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi , kulingana na ripoti ya vyombo vya habari. Taarifa hio ilisema Donald Trump Jr na wakili huyo kwanza walizungumza kuhusu upangaji wa watoto nchini Urusi mnamo mwezi Juni 2016 kulingana na gazeti la Washington Post. Bwana Trump Jr baadaye alisema kuwa amekubali kushiriki katika mkutano huo baada ya kuambiwa kwamba angepewa habari ya kumchafulia jina Hillary Clinton. Rais Trump amekana ushirikiano wowote na Urusi wakati wa kampeni. Bunge la seneti , lile la wawakilishi na mtaalam mmoja wanachunguza uingiliaji huo wa Urusi katika uchaguzi mkuu swala linalopingwa na Urusi. Gazeti la The Washington Post kwanza liliripoti kwamba rais Trump yeye mwenyewe alimfunza taarifa ambayo mwanawe alitoa kuhusu mkutano na wakili Natalia Veselnitskaya. Gazeti hilo lilitaja ...