Posts

Showing posts from October 30, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Octoba 30

Image

Anthony Joshua: Mwaka 2018 utaanza vizuri kwangu

Image
Image caption Antony Joshua akiwa na baba yake baada ya kumchapa Carlos Takam Bondia Anthony Joshua amesema upo uwezekano wa mwaka 2018 kuanza vizuri baada kumaliza 2017 kwa kumchapa Carlos Takam. Joshua bingwa wa uzito wa juu wa taji la WBA na IBF aliendeleza ushindi wake alioupata mwezi April dhidi ya Wladimir Klitschko kwa kumchapa Takam ndani ya raundi 10 mjini Cardiff. Image caption Mwamuzi alimaliza mchezo huo baada ya kuona Takam akishambuliwa kwa makonde mfululizo Mdhamini wake Eddie Hearn amesema kuna uwezekano akachauana na Deontay Wilder huku kocha wake Rob McCracken akimtaja Joseph Parker kuwa anafaa zaidi. Antony Joshua amekuwa miongoni mwa wanamichezo wanaovutia zaidi kwa siku za karibuni, huku akiweka rekodi ya kushinda kwa asilimia mia moja kwenye michuano yake yote.

Lewis Hamilton atwaa taji la nne la dunia

Image
Image caption Hamilton anasema kazi yake ni kuendesha gari na ataipenda daima Dereva Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda taji la nne la dunia katika michuano ya Mexico grand prix licha ya kumaliza akiwa nafasi ya tisa baada kugongana na Sebastian Vettel. Mafanikio ya Hamilton yanamfanya kuwa dereva wa Uingereza kufanikiwa zaidi katika historia akiwa amevunja rekodi ya Jackie Stewart. Anaungana na Vettel na mfaransa Alain Prost wenye vikombe vinne. Aligongana na Vettel wakati walipokuwa wakijaribu kupishana katika kona.

Kiongozi wa wakurdi nchini Iraq ameondoka madarakani

Image
Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES Image caption Rais wa wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amewacha wadhifa huo Rais wa wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amewacha wadhifa huo wakati eneo hilo linapambana na serikali kufuatia uhuru wake. Kupitia barua iliyosomwa kwa bunge la Kurdi, Bw. Barzani alisema kuwa hataomba kuongezwa muhula wake ambao unakamilika siku nne zinazokuja. "Ninaomba bunge kukutana ili kujaza nafasi hiyo," alisema Wakurdi walikipiga kura mwezi uliopita kuitenga Kurdistan lakini Iraq inasema kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na sheria. Kisha jeshi la Iraq likaanzisha oparesheni ya kuukomboa mji uliokuwa chini ya wakurdi wa Kirkuk na kuteka vituo vya mafuta vya mji huo. Image caption Ramani inayoonyesha Kurdistan Bwana Barzani alisema atasalia mpiganiaji wa kurdi na atazidi kutetea mafanikio ya watu wa Kurdistan. Bw Barzani aliingia ofisini mwaka 2005 baada ya kuhusika katika wajibu mkubwa wa kunda eneo huru la Kurdistan lililo kaskazin...

Mmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho

Image
Haki miliki ya picha AIIMS Image caption Mmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India. Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake. Ngugu yake, Kalia hata hivyo bado hajapata fahamu. Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha. Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa, Professor Deepak Gupta, ambaye alishiriki katika upasuaji huo aliiambia BBC. Haki miliki ya picha AIIMS Image caption Madaktari wanasema pacha hao wako hali nzuri Haki miliki ya picha AIIMS Image caption Pacha hao kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika k...

Wanawake kuruhusiwa kuingia viwanja vya michezo Saudi Arabia

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Wanawake wa Saudi Arabia kuruhusiwa kuingia viwanja vya michezo Saudi Arabia itawaruhusu wanawake kuhudhuria michezo katika viwanga vya michezo kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka ujao. Familia zitaweza kuingia kwenye viwanja vitatu vya michezo vya - Riyadh, Jeddah na Dammam. Ni hatua nyingine ya kuwapa wanawaka wa Saudi Arabia uhuru zaidi, ambao kawaida hukumbwa na ubaguzi wa kijinsia na baada ya kuendolewa marufuku ya kuendesha magari. Mfalme Mohammed bin Salman yuko katika harakati kubwa kuifanya Saudi Arabia kuwa nchi ya kisasa na kuboresha uchumi. Mabadiliko hayo yanaambatana na mipango mikubwa ya mabadiliko yaliyotangazwa na mfalme huyo wa umri wa miaka 32 kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa taifa hilo linalotegemea mafuta, yanayojulikana kama maoni ya mwaka 2030. Haki miliki ya picha AFP Image caption Wanawake wa Saudi Arabia kuruhusiwa kuingia viwanja vya michezo Mwezi uliopita amri ya kifalme ilisema kuwa wanawake...