Posts

Showing posts from June 11, 2015

WATU SITA MBARONI KWA KUKUTWA NA MIFUPA 6 YA WATU.

Image
JESHI la Polisi mkoani Tabora, limewakamata na kuwafikisha mahakamani watu sita, kwa tuhuma za kukutwa na mifupa sita ya binadamu, inayodhaniwa kuwa ni ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Suzan Kaganda alisema watuhumiwa hao walikamatwa asubuhi ya Mei 22, mwaka huu wilayani Igunga. Kaganda aliwataja watuhumiwa hao wanaodaiwa kukiri kujihusisha na matukio ya kudhuru albino kuchukua viungo kuwa ni Mussa Njile (30), mkazi wa Mnale, Elizabet Masanja (42), mkazi wa Bungwa. Wengine ni Bahati Kilungu (56), ambaye ni mwalimu na mkazi wa Mbutu Kahama, Bilia Masanja (38), mkazi wa Bukene wilayani Nzega, Muhoja John (28), mkazi wa Nyasa na Rejina Kashidye (40), mkazi wa Isegenhe. Kamanda Kaganda alikumbushia tukio la Agosti 16, mwaka jana, katika kitongoji cha Mikese kijiji cha Buhelela wilayani Igunga mkoani hapa la kuuawa kwa Mapambo Mashiri aliyekuwa amelala nyumbani kwake na mkewe, Mungu Masanja, mwen...

January makamba achukua fomu ya ugombea urahisi.

Image
Mbunge  wa jimbo la Bumbuli, mjumbe wa NEC na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba baada ya kutangaza nia  jana juni 10, amechukua fomu  katika Ofisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi mjni Dodoma  ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Makmba alisema kwamba ataendelea na safari yake  nchi nzima kutafuta wadhamini  ambao ni  wanachama wa CCM ikiwa ni sehemu ya hitaji la chama kuwa na wadhamini 450. Hata hivyo  aliwashukuru  wananchi kwa  kuungana naye  kutoka katika kila kona ya nchi  na nje ya nchi huku akisisitiza kuwa  ni zama mpya, za kizazi kipya kuamua na kujenga kesho ya nchi yetu