Posts

Showing posts from November 28, 2017

Mpelelezi wa Urusi atuhumiwa kusambaza dawa za kuongeza nguvu

Image
Image caption Grigory Rodchenkov amewahi kufanya kazi kwenye kitengo cha kupambana na dawa hizo Mpelelezi wa Urusi Grigory Rodchenkov anatuhimiwa na shirika la kupambana na dawa zilizokataliwa michezoni duniani (WADA) kwa kugawa dawa hizo kwa wanariadha wa Urusi. Serikali ya Urusi imesema kwamba wanariadha wake hawakujua kuwa Grigory Rodchenkov alikuwa akiwapa dawa ambazo zinaongeza nguvu. Rodchenkov amewahi kuwa mkuu wa kitengo cha kuzuia dawa hizo mjini Moscow. Tuhuma hizi zinakuja siku chache baada ya wanariadha wa Urusi kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Olimpiki mwaka 2018 yatakayofanyika Koreka Kusini. Awali WADA imewahi kumshutumu Rodchenkov kwa kuharibu sampuli za wanamichezo wa Urusi maksudi ili kuondoa ushahidi.

Mzee Kikwete aandika kuhusu starehe ya kustaafu “kujifanyia mambo yako mwenyewe”

Image
Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo sasa ni zaidi ya miaka miwili toka amalize miaka yake kumi ya Urais. Inaonekana J.K anapafurahia zaidi uraiani ambapo hii sio mara ya kwanza kwake kupost picha zake akiwa kwenye shughuli za kiraia mtaani. Nyingine ambayo ameiandika saa kadhaa zilizopita baada ya kuweka hizi picha ni >>>  “ Starehe ya kustaafu na kubakia kuwa raia mashuhuri ni kuweza kujifanyia mambo yako mwenyewe ikiwemo manunuzi ya mahitaji ya nyumbani”

Hii ni nyingine mpya ya kumuenzi Robert Mugabe nchini Zimbabwe

Image
Wiki moja baada ya kumuondoa madarakani, serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya  kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita. Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka. Uamuzi wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la serikali. Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa – siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37. Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF.

Gareth Bale kurejea uwanjani leo

Image
Image caption Gareth Bale amekua akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale atacheza kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne baada ya kukaa nje kwa miezi miwili. Kocha wa Madrid Zinedine Zidane amesema Bale tiyari amepona na kwa sasa yupo tiyari kurejea uwanjani kuongeza nguvu katika kikosi chake ambacho hakionekani kufanya vizuri kama misimu miwili iliyopita. Bale amekuwa nje kutokana na kupatwa na majereha ya goti na baadae nyonga na kwa sasa amejumuishwa katika timu itakayocheza na Fuenlebrada kwenye kombe la Copa del Rey. Bale raia wa Wales alionekana mara ya mwisho uwanjani walipoichapa Borussia Dortmund 3-1 kwenye kombe la klabu bingwa Ulaya. Bale ambaye pia alikosa kucheza wakati timu yake ya Wales ikisaka kufuzu kombe la dunia, hajacheza sambamba na Cristiano Ronaldo ama Karim Benzema tokea kuanza kwa msimu huu kwa sababu ya majereha ama kuwa na adhabu.

Wanariadha watano wa Urusi wafungiwa maisha

Image
Image caption Miongoni mwa wanariadha waliofungiwa Wanariadha wengine watano wa Urusi wamefungiwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Olimpiki kwa maisha yao yote baada ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuwabaini kutumia dawa zilizokataliwa michezoni. Sergei Chudinov, Aleksei Negodailo, Dmitry Trunenkov, Yana Romanova na Olga Vilukhina ndio waliokumbwa na adhabu hiyo. IOC inasema kufungiwa huko kunatokana na kamati ya 2016 ya McLaren iliyoonyesha watumiaji wa dawa hizo. Siku ya Jumatatu IOC ilitangaza adhabu hiyo na kuonya kuwa bado itaendelea kwa wale wote watakaojaribu kutumia dawa hizo.

Papa Francis aanza ziara Myanmar

Image
Image caption Papa Francis akiwa na kiongozi mkuu wa wa Myanmar Aung San Suu Kyi Papa Francis ameanza ziara yake nchini Myanmar, ambapo amekutana na mkuu wa jeshi katika siku ya kwanza ya ziara yake katika nchi inatuhumiwa kutokana na vitendo wanavyofanyiwa watu wa jamii ya Kiislam ya Rohingya. Generali Aung Hlaing ametupilia mbali madai kuwa kuna ubaguzi wa kidini katika operesheni za kijeshi zinazoendelea katika jimbo la Rakhine. Hata hivyo maofisa wengi kutoka jamii wa watu wa Budha nchini humo wanasubiria kuona kama Papa atazungumzia vipi mgogoro wa Rohingya. Kumekuwa na msukumo mkubwa dhidi ya papa Francis kutoka serikali za mataifa mengine na makundi ya haki za binadamu kuhakikisha anaweka msukumo kuhusiana na suala la Rohingya. Zaidi ya watu laki sita wamekimbia kutoka Myanmar na kwenda nchi jirani Burma na Bangaladesh tangu mwezi Agosti kutokana na mauajia yanayodaiwa kufanywa na jeshi.

Wavulana 2 wasafiri kilomita 80 chini ya basi China

Image
Haki miliki ya picha SOUTHERN MORNING POST Image caption Wawili hao ambao hawajatajwa na serikali wanatoka katika kijiji kimoja maskini Kusini mwa Guangxi na walikuwa wakijaribu kwenda kwa wazazi wao Picha za wavulana wawili wa Kichina ambao walisafiri na basi moja kwa umbali wa kilomita 80 wakiwa chini ya gari hilo zilizua hisia kali kuhusu hali ya watoto wa taifa hilo waliowachwa nyuma. Wawili hao ambao hawajatajwa na serikali wanatoka katika kijiji kimoja maskini Kusini mwa Guangxi na walikuwa wakijaribu kwenda kwa wazazi wao wanaofanya kazi katika mkoa jirani wa Guangdong. Waliripotiwa kwamba wametoweka mnamo tarehe 23 Novemba na mwalimu wao na kupatikana siku hiyohiyo chini ya gari hilo katika kituo kimoja cha mabasi. Picha na kanda za video zinaonyesha vijana hao waliojaa matope na wakining'inia chini ya basi hilo. Kulingana na gazeti la Southern Morning (Nanguo Zaobao), wavulana hao wana umri wa kati ya miaka minane na tisa na walipatikana na maafisa wa usalama...

Kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta: Usalama waimarishwa Nairobi

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Wanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais. Takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa marufuku. Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki. Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39. Sherehe hiyo ya siku ya Jumanne inayofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi inatarajiwa kuanza mwenzo wa saa nne. Waandalizi wanatarajia watu 60,000 kujaza uwanja huo...