Posts

Showing posts from September 12, 2017

''Barcelona bado ipo miongoni mwa timu mbili bora duniani''

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Ousmane Demebele na Suarez wakishangilia bao Barcelona bado ipo miongoni mwa timu mbili bora duniani licha ya kumpoteza Neymar kulingana na kocha wa Juventus Massimiliano Allegri. Juve ambao walipoteza fainali ya msimu uliopita ya kombe la vilabu bingwa dhidi ya Real Madrid inaelekea Barca siku ya Jumanne katika mechi ya kundi D. Mshambuliaji wa Brazil Neymar aliondoka na kuelekea PSG msimu huu baada ya uhamisho wake wa £200m uliovunja rekodi ya dunia. ''Pamoja na Real Madrid ni timu ambazo zina uwezo mkubwa wa kushinda ubingwa huo'', alisema Allegri. ''Wamempoteza Neymar na kumnunua kinda Ousmane Dembele , lakini pamoja na Real Madrid wanasalia kuwa timu mbili bora duniani''. Juventus iliishinda Barcelona 3-0 kwa jumla msimu uliopita katika robo fainali. Mkufunzi huyo anadhani kwamba iwapoa wataishinda Barcelona kwa mara ya tatu mfululizo itakuwa kitu muhimu sana. ''Tunajua kwamba kuchez...

Wachezaji wa Uingereza kutotumia Wi-Fi kombe la dunia Urusi

Image
Image caption Wachezaji wa Uingereza kutotumia Wi-Fi kombe la dunia Urusi kwa hofu ya kudukuliwa Wachezaji wa Uingereza na wafanyikazi wake watashauriwa kutotumia mtandao wa Wi-fi katika maeneo ya uma ama hata katika hoteli wakati wa kombe la dunia la mwaka ujao nchini Urusi kutokana na hofu ya kudukuliwa. Shirikisho la soka nchini Uingereza lina wasiwasi kwamba habari muhimu kama vile majeraha , kikosi kitakachochaguliwa pamoja na maelezo mengine ya kiufundi huenda zikadukuliwa. Hofu ya wizi wa data pia imeangaziwa kufuatia udukuzi wa mwezi uliopita uliofanywa na kundi la Fancy Bears kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku katika soka. Kundi hilo linadai kwamba habari hizo zilizofichuliwa mnamo mwezi Agosti zinaonyesha kwamba takriban wachezaji 160 walifeli vipimo vya utumizi wa dawa za kusisimua misuli 2015, huku idadi hiyo ikidaiwa kuongezeka na kufikia 200 mwaka uliofuta. FIFA inasema inaendelea kuzuia mashambulizi ya kiusalama.

Kampuni ya madini ya Petra Diamonds yasitisha uchimbaji mgodini Tanzania

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Magufuli amekuwa akisema taifa hilo linafaa kufaidi zaidi kutokana na madini Kampuni ya uchimbaji almasi ya Petra Diamonds imesimamisha shughuli zake za uchimbaji katika mgodi wake uliopo Mwadui Shinyanga, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Hii imekuja siku chache tu baada ya kamati za bunge kuwasilisha ripoti zao kwa Rais John Magufuli kufuatia uchunguzi walioufanya katika sekta ya uchimbaji madini ya almasi na tanzanite.  Petra, ambao ndio wachimbaji wakubwa wa almasi nchini Tanzania, wamekuwa wamejikuta kuwa kampuni nyingine ya kigeni kuingia katika mgogoro serikali ya Tanzania katika harakati za kufanya mageuzi katika sekta ya uchimbaji madini nchini humo. Wiki mbili zilizopita, mamlaka nchini Tanzania ziliripoti kukamatwa kwa vifurushi vya almasi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambavyo vilikuwa ni mali ya Petra na vilikuwa mbioni kusafirishwa kwenda Ubelgiji kuuzwa. Maafisa wa serikali walisema Petra il...

Kisiwa cha tajiri Richard Branson chaharibiwa na kimbunga Irma

Image
Haki miliki ya picha RICHARD BRANSON Image caption Sir Richard akitathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Irma Sir Richard Branson amesema mengi ya majengo na mimea na miti katika kisiwa chake cha Necker katika eneo la Caribbean vimeharibiwa kabisa na Kimbunga Irma. Necker ni moja ya visiwa 50 ambavyo hujumuisha Visiwa vya Virgin vya Uingereza (BVI). Sir Richard amesema alitembelea kisiwa kinachokaribia zaidi kisiwa chake cha Necker na kujionea "moja kwa moja ukali na ukatili wa kimbunga hicho". Kimbunga hicho kiliua watu watano katika eneo hilo la Uingereza. Waziri mkuu wa BVI ameomba usaidizi wa muda mrefu kutoka kwa Uingereza. Sir Richard na wenzake wako salama. Haki miliki ya picha RICHARD BRANSON Image caption Majumba katika kisiwa cha Necker yaliyumbishwa na mengine kuporomoka Kimbunag Irma kilipitia Visiwa vya Virgin vya Uingereza katikati mwa wiki iliyopita. Sir Richard amesema: "Tulihisi nguvu kali zaidi za kimbunga chenye nguvu zaid...

Uchaguzi Norway unanukia

Image
Image caption Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Norway Bi Erna Solberg kutoka katika chama cha Conservatives Utabiri rasmi kuhusiana na uchaguzi wa bunge la Norway unaonyesha kuwa zinaelekea ukingoni huku vyama viwili vikichuana vikali , kati ya chama kikuu chenye mrengo wa kati kulia na kile cha mrengo wa kushoto. Muungano wa kihafidhina wa Bi Erna Solberg unawania nafasi ya kurejea madarakani kwa kipindi cha pili.Endapo atafanikiwa atakuwa ni mwanamke wa kwanza kutoka chama cha mrengo wa kulia katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kuchaguliwa katika nafasi ya waziri mkuu. Chama cha upinzani cha Labour kinaonekana kutetea nafasi yake ipasavyo kama chama kikuu katika bunge la nchi hiyo. Kampeni za uchuzi huo mkuu zimelenga na kuzungumzia vilivyo suala la kodi, pamoja na kupunguzwa kwa ushuru kwa watunga sera ili kuongeza ukuaji wa uchumi, wakati chama cha Labour chenyewe kimejikita katika ahadi ya kuboresha huduma za umma. Bi Solberg ametawala katika ushirika n...

Korea Kaskazini yawekewa vikwazo vipya

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akikagua kiwanda cha kutengeza makombora ya Nuklia Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepiga kura kwa kauli moja kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kama adhabu ya kufanyia majaribio zana zake za nuklia. Vikwazo hivyo vinalenga kuhujumu uwezo wa Pyongyang kufadhili na kutoa kawi kwa mpango wake wa nuklya. Vikwazo hivyo vilevile vinatoa masharti kwa biashara ya kununua mafuta ya Korea Kaskazini mbali na kupiga marufuku uuzaji wa nguo katika mataifa ya kigeni. Maamuzi hayo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa yaliungwa mkono kwa wingi wa kura baada ya Marekani kuondoa mpango wake wa kutaka uungwaji mkono kutoka Urusi na China  Korea Kusini inasema kuwa kwa kuhujumu amani Korea Ksakzini itaewekewa vikwazo zaidi vya kimataifa. Balozo wa China katika Umoja wa kimataifa Liu Jieyi ameitaka Korea kaskazini kuchukua kwa muhimu mkubwa matarajio ya ya jamii ya kimataifa na kuharibu mpango...