Posts

Showing posts from September 20, 2017

Uchambuzi: Uamuzi wa Mahakama Kuu Kenya unaupa motisha upinzani

Image
Wakati jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Kenya David Maraga alipo batilisha matokeo ya uchaguzi wa Kenya alikuwa amesema kuwa alibaini "hitilafu na ukiukaji wa sheria " katika mchakato wa uchaguzi.  Uamuzi wa leo uliainisha madai yote hayo kwa kina. Mahakama imeishutumu Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) kwa kushindwa kufuata sheria katika utendaji wake.  Shutuma hiyo inakuja wakati IEBC ikikabiliwa na mzozo wa imani kwa raia.  Mahakama imeupatia upinzani silaha zaidi ya kushinikiza kufutwa kazi kwa maafisa wa tume ya IEBC na mageuzi katika mifumo uchaguzi kabla ya uchaguzi wa marudio.  Majaji wameafiki hoja ya upinzani kwamba kampuni iliyochapisha karatasi za kupigia kura, kwamba baadhi ya karatasi hizo hazikuwa na ishara za usalama. Muungano wa upinzani Nasa wanataka IEBC kuitafuta kampuni nyingine ya kuchapisha karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio.  Hii inamaanisha kwamba mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEB...

Video iliyonasa Ndege iliyobeba miili ya Watanzania 13 ikiwasili

Image
Miili ya Watu 13 wa familia moja waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea Uganda baada ya basi walilokuwa wanasafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi kugongana na lori imefikishwa Tanzania na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Messi afungia Barcelona mabao manne mechi moja La Liga

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Lionel Messi alifunga mabao manne na kuwasiadia viongozi wa La Liga Barcelona kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zote msimu huu kwa kuandikisha ushindi mkubwa dhidi ya Eibar. Messi alifunga mkwaju wa penalti na kuwaweka wenyeji hao kifua mbele kabla ya Paulinho kufunga la pili kwa kichwa. Denis Suarez kisha alifunga kutoka kwa mpira wa kudunda lakini Sergi Enrich akawakombolewa Eibar bao moja na kufanya mambo kuwa 3-1. Messi alifunga mabao mawili katika muda wa dakika moja kabla ya kubadilishana pasi murua na Aleix Vidal na kufunga bao lake la nne dakika za mwisho kwenye mechi hiyo. Ushindi huo unawaweka Barcelona uongozini wakiwa na alama 15, alama tano mbele ya Sevilla walio wa pili ingawa Barca wamecheza bao moja zaidi. Messi kwa mara nyingine anaonekana kung'aa mbele ya wavu. Image caption Messi amefunga mabao 12 mashindano yote msimu huu Mshambuliaji huyo wa Argentina amefunga mabao tisa mechi zake nne za karibuni...

Rodriguez awika mechi yake ya kwanza Bayern Munich

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES James Rodriguez alifunga bao moja na kusaidia ufungaji wa mengine mawili alipoanza mechi yake ya kwanza Bundesliga katika klabu yake mpya ya Bayern Munich. Aliwasaidia kulaza FC Schalke 04 3-0. Rodriguez, ambaye yuko Bayern kwa mkono kutoka Real Madrid ya Uhispania, alifungia Bayern bao lao la pili mechi hiyo. Katika bao la kwanza, beki Naldo alinawa krosi ya mchezaji huyo wa Colombia na kuwazawadi Bayern mkwaju wa penalti ambao ulifungwa na iRobert Lewandowski. Rodriguez aliwachenga mabeki wawili kabla ya kuupaisha mpira juu ya safu ya ulinzi ya Schalke na Arturo Vidal akafunga. Image caption Rodriguez (pili kushoto) alihamia Real Madrid kutoka Monaco kwa £71m mwaka 2014 Sven Ulreich alikuwa analinda lango la Bayern baada ya taarifa kutokea mapema jana kwamba Manuel Neuer atakwua nje ya uwanja hadi Januari baada ya kufanyiwa upasuaji mguu wake wa kushoto. Vijana hao wa Carlo Ancelotti wanaongoza ligi baada ya kushinda mechi nne ...

Leicester City wawatupa nje Liverpool Kombe la Carabao

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Islam Slimani alifunga bao la kwanza msimu huu Islam Slimani alifunga bao kwa kombora kali na kuwasaidia Leicester kuwalaza Liverpool 2-0 katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la Carabao, ambao pia hufahamika kama Kombe la EFL, uwanjani King Power Jumanne. Mchezaji huyo wa Algeria alifunga kwa mguu wa kushoto baada ya nguvu mpya Shinji Okazaki kuwaweka Leicester kifua mbele. Mabao hayo yalipatikana baada ya Liverpool kutawala kipindi cha kwanza ambapo Philippe Coutinho alikuwa amecheza vyema sana kabla ya kuondolewa uwanjani. Okazaki aliingia uwanjani na kuwaongezea nguvu Leicester na kufunga kutoka kwa pasi safi iliyotoka kwa Vicente Iborra. Alex Oxlade-Chamberlain na Dominic Solanke walionunuliwa na Liverpool majuzi wote walipoteza nafasi nzuri za kufunga. Kwingineko Roy Hodgson alipata ushindi wake wa kwanza Crystal Palace wakiwa nyumbani dhidi ya Huddersfield. Bristol City nao waliwashangaza Stoke City. Tottenha...

Nyambizi ya Ujerumani iliyozama wakati wa vita vya kwanza vya dunia yapatikana

Image
Haki miliki ya picha T TERMOTE Image caption Mchoro unaonyesha chombo kikiwa hali nzuri Mabaki ya nyambizi ya Ujerumani ambayo ilizama wakati wa vita vya kwanza vya dunia imepatikana huko North Sea na maafisa wanasema kuwa huenda bado miili 23 iko ndani ya manowari hiyo. Nyambizi hiyo ya UB-II ambayo inatajwa kuwa katika hali nzuri iko mita 30 chini ya bahari nje wa pwani ya ubelgiji. "Nyambizi hiyo iko hali nzuri na tunaamini kuwa huenda miili yote bado imo," alise gavana wa West Flanders ,Carl Decaluwé. Chombo hicho kinaamiminiwa kuzamishwa na mlipuko. Haki miliki ya picha TOMAS TERMOTE Image caption Eneo iliko nyambizi hiyo limewekwa siri kuzuia watu kulikaribia Bw. Decaluwé aliwaambia waandishi wa hababri siku ya Jumanne kuwa eneo iliko nyambizi hiyo limewekwa siri kuzuia watu kulikaribia Nyambizi 11 za Ujerumani kutoka kwa vita vya kwanza vya dunia zimepatikana katika maji ya Ubelgiji lakini chombo hiki kinatajwa kuwa kilicho katika hali nzuri za...

Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa Hotuba ya kwanza kuu ya rais wa Mareknai Donald Tump kwenye Umoja wa Mataifa imekosolewa na baadhi ya chi wanachama. Rais Trump alizitaja nchi zikiwemo Iran akisema pia kuwa Marekani itaiharibu kabisa Korea Kaskazini ikiwa italazimika kafanya hivyo. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran alisema, "hotuba ya Trump ni ya wakati ya mikutano ya wanahabari wala sio kwa Umoja wa Mataifa. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa Korea Kaskazini bado haujajibu tisho la Trump kuwa itaharibiwa. Hotuba ya Trump ilizungumzia zaidi dunia yenye mataifa huru ambayo yana malengo ya kuinua maisha ya watu wao, lakini akatumia muda mwingi akilenga kile alichokija kuwa mataifa yanayoleta matatizo duniani. Marekani mara kwa mara imeionya Korea Kaskazini kwa majaribio yake ya zana, yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. Haki mil...

Tetemeko laua zaidi ya watu 200 Mexico

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Waokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusi Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200. Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city. Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi. Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka. Haki miliki ya picha AFP Image caption Tetemeko laua zaidi ya watu 200, Mexico Daniel Lieberson alikuwa katika hotel ya Hilton Mexico City wakati tukio hilo likitokea. ''...Nilikuwa katika ghorofa ya 26. jengo lilikuwa likiyumba mbele na nyuma vioo vyote vilivunjika na tuliogopa kwamba madirisha yatavunjika, lakini haikuwa hivyo. Lakini mashine ya kutengenezea kahawa na vitu vingine vilianguka chini vyote, meza, ilikuwa shida kweli, lilidumu kwa sek...