Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Pale Unapohitaji Mkopo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Nyumba Ya Ndoto Yako.
Nimepewa siku nyingine tena ambayo napaswa niitumie vizuri kwa kadri nitakavyoweza ili iweze kuleta tija kwa maisha yangu binafsi pamoja na maisha ya kizazi hiki ndani ya nchi yetu ya Tanzania. Hii ni zawadi ya pekee ambayo thamani yake hakuna mwanadamu anaweza kuielezea pasipo na shaka ya aina yoyote. Zawadi iliyo kuu kwangu ni uzima na afya njema ambayo Mungu ameendelea kunitunuku hata muda huu ambao umenilazimu niwaambie jambo marafiki na jamaa zangu wa Tanzania. Leo napenda niwakumbushe marafiki ambao wapo kwenye hatua mbalimbali za uwekezaji wa ardhi na majengo ambao wamedhamiria kweli kufikia malengo makuu waliyojiwekea na wana mpango wa kuomba mkopo kupitia taasisi za fedha, Ni jambo jema sana kuzitumia taasisi hizi za fedha kufikia ndoto zetu kwa namna zozote vile itakavyowezekana, hii ni mbinu mojawapo ambayo baadhi ya marafiki zetu hutumia taasisi za fedha kama chanzo saidizi kwenye uwekezaji huu. Changamoto ni kwamba wengi wa marafiki wameshindwa na marafiki wachache n...