Posts

Showing posts from December 13, 2017

Tetesi za Soka Ulaya

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Olivier Giroud Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, amefichua kuwa anatathmini kuondoka huko Emirates kujiongezea fursa yake ya kuchaguliwa kujiunga na kikosi kinatachoshiriki kombe la dunia. Everton na West Ham wamehusishwa. (Sun) Lakini Arsene Wenger anasema kwa Giroud hawezi kuuzwa Januari kwa sababu anataka kumpa mshambuliaji huyo muda zaidi wa kucheza uwanjani. (Independent) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mesut Ozil Arsenal wanafanya jitihada moja ya mwisho kumshawishi Mesut Ozil kusalia kwenye klabu, wakiwa na matumaini kuwa awamu nyingine mwisho ya mazungumzo kumshawishi mchezaji huo kusalia licha ya Barcelona na Manchester United Kummezea mate. (Daily Mirror) Real Madrid bado hawajaamua kumpa ofa kipa wa Chelsea raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 25. (Sun) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption David de Gea Real licha ya kuhusishwa na mchezaji wa Manchester United David de Gea, pi...

Oscar Pistorius apata majeraha baada kupigana gerezani

Image
Image caption Oscar Pistorius (kushoto) akielekea mahakamani mwaka 2016 Mwanariadha wa zamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameumizwa mkono wake wakati akipigana gerezani wiki chache baada ya kesi ya kumuua aliyekuwa mchumba wake Reeva Steenkamp kusikilizwa tena. Mwanariadha huyo mlemavu alihusika kati ugomvi wa kugombea simu ya umma, msemaji wa gereza hilo ameiambia BBC. Pistorius aliyefungwa miaka 13 alikwaruzika ngozi ya mkono kutokana na fujo hizo. Image caption Pistorius alimpiga risasi mchumba wake Reeva Steenkamp siku ya wapendanao mwaka 2013 Hakuna majeraha mengine yaliyotajwa kumpata mwanariadha huyo. Tukio hilo lilitokea usiku wa Novemba 7, siku kumi baada ya waendesha mashitaka wa Afrika Kusini kukubali adhabu ya kifungo cha miaka sita kilichokuwa kikimkabili Pistorius kuongezwa na kuwa miaka 13.

Mugabe aondoka Zimbabwe mara ya kwanza tangu kuondolewa madarakani

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameondoka nchini humo kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa madarakani na jeshi. Bw Mugabe amesafiri kwenda Singapore kwa matibabu. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa serikali ambao wamezungumza na Reuters, Mugabe, 93, aliondoka nchini humu kwa ndege kutoka mjini Harare. Aliandamana na mke wake Grace na wasaidizi kadha. Anatarajiwa kutua mjini Malaysia ambapo binti Bona yupo akiwa mjamzito. Mugabe, aliyekuwa ameongoza taifa hilo kwa miaka 37, alijiuzulu baada ya jeshi likishirikiana na baadhi ya maafisa wakuu wa chama tawala cha Zanu-PF kumgeuka ilipobainika kwamba alikuwa anamuandaa Grace, 52, awe mrithi wake. Safari hiyo ina maana kwamba Mugabe huenda hatakuwepo nchini Zimbabwe chama cha Zanu-PF kitakapokuwa kinamuidhinisha rasmi Rais Emmerson Mnangagwa kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais wa chama hicho uchaguzi wa mwaka ujao. Chama hicho kinatarajiwa kuandaa mkutano wake mkuu Ijumaa. Ma...

Zaidi ya watoto laki nne wapo hatarini kutokana na utapiamlo DRC

Image
Image caption Wazazi na watoto wakiwa katika msururu wa kupata huduma ya afya DRC Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limeonya kuwa zaidi ya watoto laki nne walio chini ya miaka mitano wanakumbwa na utapiamlo mkubwa nchini DRC. Linasema kuwa watoto hao wanaweza kufa ndani ya miezi michache kutoka sasa kama juhudi za haraka hazitachukuliwa. UNICEF inasema mgogoro uliopo kwenye jimbo la Kasai,na kudorora kwa shughuli za kilimo ni sababu kubwa ya tatizo hilo. Hali ya usalama kwa baadhi ya maeneo ya Kongo DRC imezorota kutokana na vikundi vinavyoipinga serikali ya Kabila kufanya mashambulizi kwa wananchi na hivyo kukwamisha baadhi ya shughuli muhimu za kijamii.

Tillerson: Marekani tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini

Image
Image caption Rex Tillerson Marekani iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema. Taaarifa yake ilionekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabala ya mazungummzo yoyote kufanyika  Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wake Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika. Hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia imesababisha Marekani kuongoza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo. Kando na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Korean Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita. Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Don...

EU yajitenga na Netanyahu na Trump kuhusu Jerusalem

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Netanyahu alikutana na Federica Mogherini mjini Brussels Mkuu wa sera ya mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya (EU) amepuuzilia mbali wito wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuutaka umoja huo uutambue mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Bi Federica Mogherini amesema mataifa wanachama wa umoja huo hawataitambua Jerusalem kabla ya mwafaka wa mwisho kati ya Israel na Wapalestina kutiwa saini. Amesema EU imeungana kwa pamoja kusisitiza kwamba Jerusalem inafaa kuwa mji mkuu wa Israel na pia taifa la Wapalestina litakapoundwa. Alikuwa akihutubu baada ya mkutano ambapo Bw Netanyahu alitoa wito kwa EU kuifuata Marekani katika kuitambua Jerusalem. Hatua ya Rais wa Marekani kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel imeshutumiwa vikali na Wapalestina na pia jamii ya kimataifa. Aidha, imeyakera sana mataifa ya Kiarabu na Kiislamu. Maandamano yameshuhudiwa katika maeneo ya Wapalestina Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, na pia kat...