Posts

Showing posts from December 5, 2017

Ghoulam ajitia kitanzi Napoli mpaka 2022

Image
Haki miliki ya picha GOOGLE Image caption Faouzi Ghoulam aongeza mkataba wake na Napoli Beki wa kimataifa wa Algeria anayekipiga na klabu ya Napoli, Faouzi Ghoulam ameongeza mkataba na klabu yake utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2022. Mkataba wa sasa wa mlinzi huyo unamalizika tarehe 30 ya mwezi june mwaka 2018, hivyo mkataba mpya umeongeza miaka minne ya wa kukipiga na vinara wa Seria A. Ghoulam kwa sasa anauguza jeraha la goti alilofanyiwa upasuaji baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Manchester City. Beki huyo alijiunga na Napoli mwaka 2014, akitokea Saint Etienne ya nchini Ufaransa na amekwisha cheza michezo 153 katika kablu hiyo

Urusi yafungiwa kushiriki michuano ya olimpiki

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Nembo ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, imeifungia nchi ya urusi kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itayofanyika katika jiji la Pyeongchang nchini Korea kusini mwakani. Rais wa IOC Thomas Bach na bodi yake walitangaza adhabu hiyo jana jioni baada ya kukutana katika mji wa Lausanne nchini Switzerland, maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa miezi kumi na saba. Serikali ya Urusi ilihusika katika udanganyifu wa kuanda michuano ya olimpiki iliyofanyika nchini humo mwaka 2014 pamoja na udanganyifu kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni. Uchunguzi huo ulikuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa IOC Samuel Schmid, Licha adhabu hiyo wanariadha wa Urusi wanaweza shiriki michuano ya majira ya baridi kama wanaridha huru ambao watakuwa wakiwakilisha nchi.

Onyo jipya kuhusu Trump kuutambua mji wa Jerusalem latolewa

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Onyo jipya kuhusu Trump kuutambua mji wa Jerusalem latolewa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuambia Donald Trump kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa Marekani anaweza kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Uamuzi wowote kuwa mji huo unastahili kuwa katika viwango vya mazungumzo kati ya Israel na Palestina, Bw Macron alisema. Mapema onyo kama hilo lilitolewa na nchi za kiarabu na mataifa ya kiislamu. Ripoti zinasema kuwa rais wa Mareknia atautambua mji wa Jerusalem kuwa mji wa mkuu wa Israel. Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu. Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES Image caption Rais Macron alimpigia Trump simu kuelezea wasi wasi wake Ikulu ya White House iliseam kuwa anaweza kukosa siku ya mwisho ya Jumamosi kuweka sahhihi agizo la kuzuia kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Avivi kwenda Jerusalem. Kila rais akiwemo Trump ametia sahhihi agizo kila baada ya miezi sita tangu bunge le Co...

MAGAZETI YA TZ NA NJE LEO DECEMBER 5,2017

Image

Mahakama nchini Marekani yaruhusu kutekelezwa marufuku ya usafiri ya Trump

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Vizuizi vya wageni kutekelezwa Mahakama kuu nchini Marekani imeamua kuwa toleo la marufuku ya kusafiri ya Rais trump inaweza kutekelezwa kwa ukamilifu. Huku ikiendelea kukutana na changamoto za kisheria kutoka mahakama za chini.  Nchi sita zinazokutana na zuio hilo ni Iran, Libya, Syria, Yemen, Somalia na Chad.Mahakama za chini tayari zimeruhusu kuzuiwa kwa baadhi ya watu kutoka Korea kaskazini na Venezuela. Majadiliano Zaidi yatendelea kusikilizwa wiki hii katika mahakama huko San Francisco, California, na Richmond, Virginia. Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kwamba, kwa sasa, huu ni ushindi mkubwa kwa Donald Trump. Msemaji wa Ikulu ya White Hogan Gidley alisema kuwa White House haikushangazwa na uamuzi wa mahaka ya juu. Mwanasheria mkuu Jeff Sessions aliutaja uamuzi huo kama ushindi mkubwa kwa usalama wa watu wa Marekani.

Mwanafunzi Aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel za UDSM Atiwa Mbaroni

Image
  Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson anashikiliwa na polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya hosteli. Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) alikamatwa jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana. Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo jana saa saba mchana. "Ni kweli Kumbusho alikamatwa jana mchana  na kupelekwa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo wakampeleka Oysterbay," amesema Anastazia. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo. Alisema anasubiri atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.