Posts
Showing posts from December 10, 2017
Rais Magufuli awasamehe wafungwa 61 wa kunyongwa
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Rais Dkt John Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa wa kunyongwa na wale maisha. Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake. Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha
Mataifa ya Kiarabu yataka kuiwekea Marekani vikwazo vya Kiuchumi
- Get link
- X
- Other Apps
Jana Jumamosi kulishuhudiwa ghasia katika mji wa Nablus, West Bank Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES Image caption Siku ya Jumamosi kulishuhudiwa ghasia katika mji wa Nablus, West Bank Mataifa ya kiarabu yameitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake wa kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli. Kwa njia ya taarifa walioitoa kwa kauli moja kwenye mkutano wao Mjini Cairo- Misri, muungano huo umesema kuwa hatua hiyo ni hatari na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na litaitumbukiza mataifa ya mashariki ya kati katika ghasia mbaya. Mawaziri kwenye mkutano huo, sasa wanaiomba jamii ya kimataifa kutaja Mashariki mwa Jerusalem kama makao makuu ya Palestina. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Lebanon, Gebran Bassil, amesema kuwa mataifa ya kiarabu, yanafaa kufikiria hatua ya kuiwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi, ili kuizuia kuhamishia makao makuu ya Israeli hadi Jerusalem, kutoka Tel- Aviv. Bwana Bassil, amesema kuwa, hatua za kidiplomasia na kisiasa, zinafaa ku...
Katibu mkuu wa CUF Maalim seif hamad ametuma salamu za lambi lambi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.John Pombe Magufuli.
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuomboleza vifo vya askari 14 waliouawa nchini Kongo na wengine kujeruhiwa, huku akiwapa pole wafiwa wote. Kufuatia msiba huo Maalim Seif ametuma salamu za rambirambi kwa Rais Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Maafisa na Askari wote wa JWTZ, familia na ndugu wa marehemu na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuwapoteza mashujaa waliokuwa wakitekeleza wajibu wao kwa niaba ya Taifa. "Natuma salamu zangu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waathirika wote na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kwa wale waliojeruhiwa nawatakia uponaji wa haraka ili warejee katika majukumu yao ya kawaida, na tunawaombea marehemu wote Mwenyenzi Mungu awapumzishe mahala pema peponi", amesema Maalim Seif. Pamoja na hayo Maalim Seif...
Zanzibar Heroes Hawakamatiki...Yafuzu Hatua ya fainali ya CECAFA Senior Challenge
- Get link
- X
- Other Apps
Timu ya taifa ya kandanda ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya fainali ya CECAFA Senior Challenge baada ya kutoka suluhu na Kenya jioni hii. Mchezo huo umemalizika jioni hii kwenye uwanja wa Kenyatta uliopo County ya Machakos ambapo Zanzibar Heroes imeilazimisha suluhu ya 0-0 timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars. Zanzibar Heroes imefuzu hatua hiyo baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Rwanda na Kilimanjaro Stars na kutoka sare moja ya leo dhidi ya Kenya, hivyo kuongoza kundi A. Zanzibar Heroes sasa imefikisha alama 7 na kufuzu hatua hiyo ikifuatiwa na Kenya yenye alama 5 ambayo itasubiri matokeo yake ya mchezo wa mwisho dhidi ya Kilimanjaro Stars. Mapema mchana leo timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imetolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 2-1 na timu ya taifa ya Rwanda.