Posts

Showing posts from December 18, 2017

Kaka: Nyota wa zamani wa Brazil na AC Milan atangaza kustaafu

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Kiungo wa kati wa zamani wa AC Milan na Real Madrid Kaka ametangaza kustaafu soka. Kaka alishinda Kombe la Dunia mwaka 2002 akiwa an Brazil. Mchezaji huyo wa miaka 35 alianza uchezaji soka wake Brazil akiwa na klabu ya Sao Paulo, na amekuwa akichezea Orlando City inayocheza Ligi Kuu ya Amerika ya Kaskazini (MLS). Kaka alicheza mechi yake ya mwisho Oktoba Orlando walipomaliza msimu, na mwezi Novemba taarifa zilisema alikuwa amepewa kazi ya kuwa mkurugenzi katika klabu ya AC Milan. Yeye ni miongoni mwa wachezaji wanane pekee waliowahi kushinda Kombe la Dunia, Kombe la Ulaya/Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na tuzo ya Ballon d'Or.  Wengine ni Bobby Charlton, Gerd Muller, Franz Beckenbauer, Paolo Rossi, Zinedine Zidane, Rivaldo na Ronaldinho. Kaka alichezea Brazil mechi 92 na kuwafungia mabao 29. Baada ya kushinda Kombe la Dunia, alishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Milan mwaka 2007 na akakabidhiwa tuzo ya Ballon d'Or (tuzo ...

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi

Image
Haki miliki ya picha @ANTOINEGRIEZMANN Image caption Griezmann aliifuta picha hiyo kutoka kwenye ukurasa wake wa Twitter na kisha akaomba radhi Mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann ameomba radhi baada yake kushutumiwa vikali kwa kujipaka rangi nyeusi kama sehemu ya utani wa kubadilisha sura. Alikuwa awali amewaambia wafuasi wake kwenye Twitter watulie kabla ya kulazimika kuchukua hatua hiyo. Griezmann alikuwa amepakia kwenye Twitter picha yake akiwa amevalia kama mchezaji mweusi wa mpira wa kikapu. Baadaye aliifuta picha hiyo, sawa na ujumbe wa pili aliokuwa ameuandika uliosema: "Tulieni nyote. Mimi ni shabiki wa Harlem Globetrotters na natoa heshima kwao." Ujumbe wake wa tatu ulikuwa wa kuomba radhi. Aliandika: "Natambua kwamba nilikowa kumakinika. Iwapo nimewakera baadhi ya watu, basi naomba radhi." Mbunge wa chama cha Labour UIngereza David Lammy alikuwa miongoni mwa waliomshutumu Griezmann.  Aliandika kwenye Twi...

Taarifa kuu Jumatatu 18.12.2017: Washindi wa urais Chile na Honduras watangazwa, Trump ajitetea

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Kulikuwa na utata awali kuhusu utaratibu wa kupiga kura chama cha ANC Afrika Kusini Mfanyabiashara mhafidhina Sebastian Pinera ameshinda uchaguzi wa urais Chile, Juan Orlando Hernandez naye akatangazwa mshindi Honduras. Afrika Kusini chama cha ANC nacho kinamchagua kiongozi wake: Hizi hapa ni taarifa kuu leo kimataifa: Mrithi wa Zuma chama cha ANC kujulikana leo Haki miliki ya picha REUTERS/AFP Image caption Kuna ushindani mkali kati ya Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril Ramaphosa Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kinapiga kura kumchagua atakayemrithi rais Jacob Zuma kama kiongozi wa chama hicho. ANC kilisema kimebadilisha uamuzi wake wa awali kuchelewesha kura hiyo hadi leo Jumatatu. Takriban wajumbe elfu tano wanamchagua kati ya makamu wa rais Cyril Ramaphosa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Nkosazana Dlamini-Zuma. Pinera ashinda urais Chile Haki miliki ya picha MARTIN BERNETTI Image caption Sebastián Piñera ataongoza ...

ANC inamchagua kiongozi mpya Afrika Kusini

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Wagombea ni makamu wa rais Cyril Ramaphosa na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa Bw Zuma Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimewaidhinisha wagombea wawili kuwania kumrithi Rais Jacob Zuma katika uongozi wa chama. Wagombea hao ni makamu wa rais Cyril Ramaphosa na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa bwana Zuma. Kumekuwa na mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura. Uwaniaji madaraka umeleta mvutano mkubwa wa kisiasa, hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019. Rais Zuma ameonya kuwa chama kimo hatarini na kimo kwenye njia panda. Haki miliki ya picha AFP Image caption ANC Zaidi ya wajumbe 5,000 wanashiriki katika mkutano wa siku nne katika ukumbi wa Expo Centre mjini Johannesburg. Kwa namna inavyoonekana, Bw Ramaphosa ana wafuasi 1,469 kulinganisha na 1,094 wa mke wa zamani wa Rais Zuma, Bi Dlamini-Zuma. ...

Mrisho Ngossa Arudi Mbeya City Kudai Chake

Image
Ngassa LICHA ya kutua Ndanda FC, kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa amepanga kurejea kwenye timu hiyo kwa ajili ya kudai malipo yake ya mshahara. Kiungo huyo, amejiunga na Ndanda hivi karibuni katika usajili wa dirisha dogo lililofungwa Ijumaa iliyopita. Akizungumza na Championi Jumatatu, Ngassa alisema hajaachwa kama watu wanavyosema, isipokuwa mkataba wake Mbeya City ulimalizika. Ngassa alisema, anashukuru ameondoka kwa amani katika timu hiyo na kikubwa amepanga kurejea katika timu hiyo kwa kudai malimbikizo yake ya fedha ikiwemo mshahara wake. Aliongeza kuwa, hivi sasa anajiandaa kwa ajili ya kwenda kukutana na changamoto mpya katika timu yake ya Ndanda katika mzunguko wa pili wa ligi kuu. “Ni jambo jema kwangu kuondoka kwa amani kabisa Mbeya City na ninashukuru nimemalizana nao salama mara baada ya mkataba wangu wa miezi sita kumalizika. “Lakini nikiwa naenda zangu Ndanda kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo, nimepanga kurejea tena Mbeya kwa ajili ya kudai m...