Posts

Showing posts from September 13, 2017

Saimon Msuva mchezaji bora wa Agosti

Image
Haki miliki ya picha GOOGLE Image caption Simon Msuva mchezaji bora wa mwezi August wa ligi kuu ya Morocco Mtanzania Saimon Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Agosti katika klabu yake inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco. Msuva ambaye anakipiga Difaa Al Jadid ameteuliwa kuwa mchezaji wa Agosti kutokakana na mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo. Msuva amejiunga na timu hiyo miezi miwili iliyopita akitokea Yanga ya Tanzania na tayari ameonekana kuwa tegemeo katika ufungaji wa mabao katika kikosi hicho.Msimu uliopita, Difaa Al Jadid ilishika nafasi ya pili, hivyo msimu huu itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezaji ghali duniani aisaidia PSG kuicharaza Celtic 5-0

Image
Image caption Cavani, Mbappe na Neymar Klabu ya Celtic ilipokea kichapo kikubwa zaidi nyumbani huku Neymar akiiongoza PSG katika kombe la vilabu bingwa Ulaya. Neymar ambaye ndio mchezaji ghali duniani aliifungia timu yake mpya na kusaidia kupatikana kwa bao la pili ambalo lilifungwa na Kylian Mbappe. Edison Cavani alifunga bao la tatu kwa njia ya penalti na hivyobasi kuwahkikishia wageni hao uongozi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza. Bao alilojifunga Mikael Lustigs lilifuatiwa na bao la pili la Cavani ambalo lilifungwa kupitia kichwa kizuri. Celtic imekuwa mwenyeji wa timu kubwa za bara Ulaya katika kombe hilo katika miaka ya hivi karibuni, lakini hata wale waliokuwepo katika zama za klabu hiyo hawajawahi kushuhudia kipigo kama hicho cha 5-0. Kasi yao, mafikira na mchezo wao ulikuwa wa kiwango cha hali ya juu.

Raia wa Burundi ''waliotaka kujiunga na al-Shabab'' wamakatwa

Image
Image caption Wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia Police nchini Kenya wamewakamata watu wanne wanaoaminika kuwa raia wa Burundi ambao walikuwa wakielekea Somalia kujiunga na kundi la al-Shabab. Maafisa wa ujasusi walikuwa wakiwafuata washukiwa hao baada ya kupata habari kuhusu mipango yao, kulingana na msemaji wa polisi George Kinoti. Ameongezea kwamba washukiwa wanne walikamatwa katika kizuizi cha polisi mjini Isiolo takriban kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu wa nairobi wakielekea katika mji wa mpakani wa Mandera. Maafisa wa polisi pia wanasema wanne hao waliingia nchini Kenya kama watalii kupitia visa huru ya ushirikiano kati ya Burundi na Kenya. Maafisa katika Ubalozi wa Burundi mjini Nairoibi wanasema kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu kukamatwa huko baada ya kushauriana na mamlaka ya Kenya. Mnamo mwezi Januari mwaka huu raia mwengine wa kigeni, ambaye alikuwa Mtanzania alikamatwa mjini Mandera akijaribu kuvuka na kuingia Somalia kwa lengo la kujiunga na kundi ...

Utafiti: Kilimo cha kupindukia chanzo cha majangwa

Image
Image caption Utafiti wa umoja wa mataifa umebaini kuwa thuluthi moja ya ardhi kote duniani imeharibiwa na shughuli nyingi za kilimo kupindukia Utafiti wa umoja wa mataifa umebaini kuwa thuluthi moja ya ardhi kote duniani imeharibiwa na shughuli nyingi za kilimo kupindukia Utafiti huo unaonyesha kwamba udongo usiokuwa na rutuba unatishia kuzua baa la njaa kwa mamilioni ya watu pamoja na kuleta umaskini na mizozo. Umoja wa mataifa unasema tani bilioni ishirini na tano za udongo wenye rutuba na miti bilioni kumi na tano hupotea kila mwaka. Umesema kuwa sera za kitaifa za kuzuia ardhi kubadilika na kuwa jangwa ni muhimu katika kuzuia kile inachodai huenda kikawa chanzo cha migogoro lakini ukaongezea kuwa uhifadhi wa chakula pia unaweza kusaidia. Utafit huo umebaini kwamba ukulima unaofanywa na viwanda ambapo mashine kubwa hutumiwa kulima na kuvuna hupunguza rutuba ya udongo kwa kiwango kikubwa.

Raia wa Burundi ''waliotaka kujiunga na al-Shabab'' wamakatwa

Image
Image caption Wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia Police nchini Kenya wamewakamata watu wanne wanaoaminika kuwa raia wa Burundi ambao walikuwa wakielekea Somalia kujiunga na kundi la al-Shabab. Maafisa wa ujasusi walikuwa wakiwafuata washukiwa hao baada ya kupata habari kuhusu mipango yao, kulingana na msemaji wa polisi George Kinoti. Ameongezea kwamba washukiwa wanne walikamatwa katika kizuizi cha polisi mjini Isiolo takriban kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu wa nairobi wakielekea katika mji wa mpakani wa Mandera. Maafisa wa polisi pia wanasema wanne hao waliingia nchini Kenya kama watalii kupitia visa huru ya ushirikiano kati ya Burundi na Kenya. Maafisa katika Ubalozi wa Burundi mjini Nairoibi wanasema kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu kukamatwa huko baada ya kushauriana na mamlaka ya Kenya. Mnamo mwezi Januari mwaka huu raia mwengine wa kigeni, ambaye alikuwa Mtanzania alikamatwa mjini Mandera akijaribu kuvuka na kuingia Somalia kwa lengo la kujiunga na kundi hi...