USHAURI; Hatua Muhimu Za Kuchukua Ili Kuondoka Kwenye Madeni Na Kuongeza Kipato Chako.
Karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto ambazo zinatuzuia kuwa na maisha ya mafanikio. Changamoto ni nyingi, zipo zinazotokea kutokana na mazingira na pia zipo ambazo tunatengeneza sisi wenyewe, kwa kujua au kutokujua. Kwa vyovyote vile, tunapaswa kutatua changamoto zozote tunazokutana nazo ili kuweza kufanikiwa. Leo tunakwenda kuangalia changamoto ya madeni na kipato kuwa kidogo. Hivyo tutaangalia ni jinsi gani mtu unaweza kuondoka kwenye madeni na kuweza kuongeza kipato chako ili kuondokana na changamoto za kifedha. Kabla hatujaingia ndani na kuona hatua za kuchukua, tusome maoni ambayo msomaji mwenzetu ametuandikia; Nashukuru kwenye makala ya leo uliyoonesha njia ya kuepukana na kujipa presha na wakopaji wasio waaminifu. Umetoa ushauri ambao nimewahi kuutumia, jirani alikopa kwangu sh.20,000/= akaanzisha meza ya nyanya, hajanirudishia pesa hadi sasa lakini ni kweli kuwa sasa haombi kitu kutoka kwangu tena. Lakini kocha mimi nina tat...