Hospitali ya watoto ya Hunan nchini China yawafunda madaktari na wauguzi wa Zanzibar
Makamu wa Rais wa Hospitali ya Watoto ya Hunan nchini China akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku 10 ya Madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto katika Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Mnazimmoja mafunzo yanayofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Balozi mdogo wa china aliepo Zanzibar XieXiawu akitoa hutuba katika ufunguzi wa mafunzo ya siku 10 ya kuwajengea uwezo madaktari na wauguzi wanaofanyakazi wodi za watoto za Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Kivunge. Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akifungua mafunzo ya madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto na kuimarisha utawala wa Hospitali, mafunzo yanayofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja. Washiriki wa mafunzo kutoka Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na Makunduchi wakiwa pamoja na wakufunzi wao kutoka Hospitali ya Hunan China wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Naibu Waziri wa Afya Bi. Arusi Said Suleiman (hayupo pichani). ...