Posts

Showing posts from December 14, 2017

Furry ataka kuzipiga na Anthony Joshua

Image
Image caption Furry ni miongoni mwa mabondia wa Uingereza waliotamba mwaka 2015 Bondia wa uzito wa juu wa Uingereza Tyson Fury ametaka kupewa pambano la haraka baada ya kurejea tena katika ndondi. Fury aliyefungiwa kushiriki mchezo huo mwaka 2016 kwa sababu sampuli zake zilisemekana kuonyesha kutumia dawa za kusisimua misuli, ametaka pia kurudishiwa mikanda yake mara moja. Bondia huyo mwenye miaka 29 tiyari ameonyesha nia ya kupambana na mkali wa uzito wa juu Anthony Joshua mwaka 2018. Promota wa Joshua, Eddie Hearn amesema ni jambo jema na anaamini Furry atachapwa ndani ya raundi tano. Furry alipatikana na hatia ya kutumia dawa zilizokataliwa michezoni na kwa sasa adhabu yake inafikia ukingoni.

Mwanamke aliyejaribu kuwauza watoto wake pacha akamatwa Nigeria

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda cha watoto" katika jimbo la Imo Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya madai kuwa alijaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja nchini Nigeria. Ameshtaki kwa kuhusika katika bishara ya kuuza watoto lakini polisi wanasema kuwa mashtaka zaidi yataongezwa. Mwanamke huyo alikamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake wasicha kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi. Visa vya kuuzwa watoto wa kupangwa vimekuwa tatizo kwa muda mrefu chini Nigeria. Image caption Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini. Alipohojiwa mwanamke huyo alisema kuwa changamoto za kifedha zilisababisha afanye hivyo. Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini. Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 1...

Mwanamke aliyemuua mume wake ili aishi na mpenzi wake India

Image
Image caption Swati Reddy (kulia) na mpenzi wake wanadaiwa kumuua mume wake Sudhakar (kushoto) mwezi uliopita Wapenzi wiwili nchini India wamekamatwa kwa kumuua mume wa mwanamke na kisha kujaribu kumfanyia upasuaji wa kubadilisha sura mwanamume mpenzi ili aweze kuchukua mahala pake, Tindi kali ilimwagwa kwenye uso wa mwanamume, mpenzi wa mwanamkea, katika shambulizi lililopangwa, huku wapenzi hao wakipanga kusema kuwa sura yake ilikuwa imebadilika baada ya upasuaji. Lakini ndugu wa bwana wa mwanamke aligundua mpango huo alipofika hospitalini. Alitoa malalamiko yake kwa polisi ambao walifanya uchunguzi wa vidole na kugundua njama huyo. Mke, Swati Reddy amekamatwa. Polisi waliiambia BBC kuwa watamkamata pia mpenzi wake, Rajesh Ajjakolu mara atakapotibiwa majeraha yake na kuruhusiwa kuondoka hospitalini. Image caption Rajesh Ajjakolu alilazwa hospitalini akiwa na majeraha ya uso Bwana Sudhakar Reddy anadaiwa kuuliwa usiku wa tarehe 26 Novemba na mwili wake kutupwa siku i...

Mwanamume asiye na makao apata pesa nyingi uwanja wa ndege Ufaransa

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mwanamume asiye na makao apata pesa nyingi uwanja wa ndege Ufaransa Mwanamume ambaye alipata puani 260,000 baada ya kuegemea mlango wa kampuni ya Charkles de Gaulle kwenye uwanja wa ndege nchini Ufaransa anaaminiwa kuwa mtu asiye na makao. Polisi wanasema kuwa walimtambua mwanamume huyo kupitia kwa kamara za cctv kama mmoja wa watu wanaolala karibu na uwanja wa ndege. Mlango wa kampuni inayoshughulikia masuala ya fedha ya Loomis terminal 2F, ulikuwa umeachwa bila kufungwa na mwanamume ambaye umri wake unatajwa kuwa wa miaka 50 hivi alitoka nje akiwa na mifuko miwili ya pesa. Kwa sasa anasakwa na polisi. Mwendo wa saa (16:30 GMT) Ijumaa iliyopita king'ora kililia katika kampuni hiyo inayohusika na masuala ya fedha. Maafisa waliochunguza video ya cctv waligundua kuwa mwananammue huyo alikuwa akitafuta kwenye ndoo za taka nje ya ofisi hizo, na kuonekaka kushangazwa wakati mlango aliokuwa ameegema ulipofunguka. Aliingia ...

Israel yaendeleza mashambulizi dhidi ya Hamas kujibu mashambulizi kutoka Gaza

Image
Image caption Israel na Hamas waendeleza mapambano kis mji wa Jerusalem Jeshi la Israel limesema mashambulizi yake roket yanazilenga ngome tatu za kijeshi za wapiganaji wa kundi la Hamas,ikiwa ni hatua ya kujibu shambulizi dhidi yao la kutoka ukanda wa Gaza. Israel pia imeamuru kufungwa kwa mpaka kati yake na Gaza,baada ya shambulizi la nne maroketi yanayodaiwa kurushwa na kundi la HAMAS. Hali hii ya mapigano ya kundi la Hamas inadaiwa kuwa ni kutokana na hasira kufuatia hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jesrusalem kama makao makuu ya Israel. Hata hivyo jeshi la Israel linasema kuwa makombora kati ya yaliyorushwa,walifanikiwa kuyazuia,ambapo moja lilianguka eneo la wazi kusini mwa Israel na jingine lilipoteza uelekeo.