Posts

Showing posts from August 10, 2017

Mfumuko wa bei washuka nchini.

Image
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa kipindi cha Julai mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwapo mwezi Juni mwaka huu hali inayomaanishakasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa imepungua. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo, amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa kipindi cha Julai mwaka huu kumechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2017 ikilinganishwa na bei za Juni 2016. “Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama, kwa asilimia 16.6, bilinganya (10.6), vitunguu (13.2), karoti (16.9) na viazi mviringo (13.5)"  amesema. Aidha ameeleza kuwa Shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika ambapo uwezo wa Shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma ulifikia Shilingi 91 na senti 87 kipindi cha Julai 2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na senti 66 ilivyo...

Korea Kaskazini: Tuna mpango wa kushambulia kisiwa cha Marekani cha Guam siku chache zinazokuja

Image
Haki miliki ya picha Image caption Korea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam Korea Kaskazini inasema mpango wake ya kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya kivita kati yake na Marekani yakiendelea. Vyombo vya habari vilisema kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa mpango huo utaidhinishwa na Kim Jong-un. Korea ilipuuzna onyo la Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali. Marekanai imeionya Korea Kaskazini ikisema kuwa vitendo vyake vinamaanisha kuwa huo utakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo. Image caption Kisiwa hicho kilicho bahari ya Pacific cha Guam ndiko ziliko kambi za jeshi za Marekani na watu 163,000 Waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis alisema kuwa Korea Kaskazini itashindwa vibaya ikiwa itaingia vitani na Marekani na washirika wake. Korea Kaskazini ilitangaza si...

Uchaguzi Kenya: Matokeo kamili ya urais yasubiriwa

Image
Ni siku ya tatu sasa tangu Wakenya walipofika katika vituo vya kura kuwachagua viongozi na matokeo kamili ya uchaguzi wa urais yanaendelea kusubiriwa Tume ya Uchaguzi inaendelea kupokea Fomu 34A za matokeo ya urais kutoka vituoni Matokeo ya awali yanaonesha Rais Kenyatta anaongoza akiwa na kura 8 milioni. naye Bw Odinga ana kura 6.6 milioni. IEBC imesema mitambo yake haidukuliwa, kinyume na madai ya muungano wa upinzani Nasa Jumanne kulitokea vurugu katika baadhi ya maeneo mtaa wa Mathare, Nairobi na baadhi ya maeneo Kisumu. Lakini kwa sasa hali ni tulivu Waziri wa usalama Fred Matiang'i amewaomba wananchi kuendelea na shughuli za kawaida bila wasiwasi Katika barabara za Nairobi magari yameanza kuonekana lakini bado hali ya kawaida haijarejea Yasemavyo magazeti Kenya leo Imepakiwa mnamo 8:35 Hivi ndivyo magazeti nchini Kenya yalivyoangazia matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne, hatua ya upinzani kupinga matokeo ya awali yanayotangazwa, kutokea kwa...