Posts
Showing posts from December 21, 2017
Swansea City yamtimu kocha Paul Clement
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo msimu huu. Clement mwenye miaka 45 alichukua jukumu la kuiongoza Swansea, mwezi Januari mwaka huu na kuisaidia kutoshuka daraja na kumaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita. Katika msimu huu mpaka sasa Swansea wamecheza michezo 18, na wameshinda michezo mitatu ya ligi wakiwa wanaburuza mkia kwa alama 12. Mwenyekiti wa Swansea Huw Jenkins, ametoa taaarifa kwa kusema klabu imelazimika kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia timu kufanya vizuri.
Bristol City yaitupa nje ya michuano Man United
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao kwa kuwaondosha mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Manchester United. Bristol walianza kuzifumania nyavu za United kwa goli la Joe Bryan, katika dakika ya 51 ya mchezo iliwchukua dakika saba tu kwa Manchester United, kusawazisha goli hilo kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic. Shujaa wa Bristol City alikuwa ni kiungo Korey Smith aliyefunga goli la ushindi katika dakika za lala salama. Nayo Chelsea wakatinga katika hatua ya nusu fainali kwa kuwatungua AFC Bournemouth kwa magoli 2-1 . Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mfungaji wa bao la Chelsea Kiungo Willian Borges da Silva, ndie aliyeanza kupatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 13 ya mchezo Bournemouth wakasawazisha goli hilo katika dakika ya tisini kupitia kwa kiungo Daniel Gosling, Mshambulia...
Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun kuzikwa leo
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Kim Jong-hyun alikua mwanamuziki mashuhuri Korea Kusini Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul. Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alikutwa amekufa katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua. Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu. Image caption Picha yake iliwekwa hospital mjini Seoul Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul. Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee,alikutwa ameanguka kutoka ghorofa moja refu la kupangisha siku ya Jumatatu.
Trump awatishia watakaounga mkono maazimio ya UN juu ya mji wa Jerusalem
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Trump;"Waache wapige Kura dhidi yetu. Tutahifadhi fedha yetu vya kutosha. Hatujali" Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kusitisha misaada ya kifedha kwa nchi ambazo zinaunga mkono maazimio ya umoja wa mataifa ya kupinga Jerusalem kutambulika kama mji mkuu wa Israel. Mapema mwezi huu, Bwana Trump alichukua uamuzi huo licha ya kukabiliwa na ukosolewaji mkubwa kutoka mataifa mbalimbali. "Wanachukua mamia ya mamilioni ya dola na hata bilioni za dola kisha wanapiga kura dhidi yetu" aliwaambia wanahabari katika White House. "Waache wapige Kura dhidi yetu. Tutahifadhi fedha yetu vya kutosha. Hatujali" Maneno yake hayo yanakuja baada ya Mkutano wa Umoja wa mataifa kupiga kura kupinga hatua yoyote ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Haki miliki ya picha EPA Image caption Mkutano wa Umoja wa mataifa kupinga hatua yoyote ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Muswada wa maazimio haukuitaja Marekani lakini unas...
Uganda yaondoa kikomo cha umri wa kugombea urais
- Get link
- X
- Other Apps
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Rais Yoweri Museveni sasa anaweza kuwania urais tena mwaka 2021 Wabunge wa Uganda wameyapitisha mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita. Baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini kutokana na kuupinga muswada. Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu. Haki miliki ya picha BUNGE LA UGANDA Image caption Wabunge wa Uganda Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mita...
Ramaphosa ahaidi kuimarisha uchumi wa Afrika Kusini
- Get link
- X
- Other Apps
Image caption Cyril Ramaphosa amekuwa kiongozi mkuu wa ANC baada ya kuwashinda wapinzani wake akiwemo Nkosazana Dlamini Zuma Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo. Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake. Image caption Ramaphosa na Zuma awali walikua marafiki wa karibu Amesema kuwa kikao cha kamati kuu kimeahisi pia kurudisha ardhi muhimu ambazo zilikua mikononi mwa wasiohitajika ikiwa ni lengo la kukuza sekta ya kilimo. Amemsifu mpinzani wake wa kaziribu ayembwaga kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa ANC Nkosazana Dlamini Zuma kuwa ni jasiri na mchapa kazi.
Rais Dkt Magufuli amteua Wakili Albert Msando Katika tume kuchunguza mali za CCM
- Get link
- X
- Other Apps
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi apata ajali, avunjika mkono na Kulazwa hospitali ya KCMC
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi baada ya kuvunjika mkono. Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amevunjika mkono wa kushoto baada ya kuteleza na kuanguka na amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP). Msaidizi wa mbunge huyo, Hamis Hamis alisema jana Jumatano Desemba 20,2017 kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2:45 usiku wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani. Hamis alisema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka. “Bahati nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaitwa Ansbert Sweetbert ndiye alitoa huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” alisema. Alisema, “Kwa kweli huyo daktari alikuwa msaada mkubwa. Ndiye aliyempeleka KCMC na alikaa naye hadi saa nane usiku. Wauguzi na madaktari KCMC walimpa msaada mkubwa.”