Posts

Showing posts from August 9, 2017

Matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya

Muungano wa upinzani Nasa umepinga matokeo yanayotangaza na kusema IEBC imekuwa ikitangaza matokeo bila kutoa fomu 34A Kumekuwa wagombea urais wanane, lakini ushindani mkubwa ulikuwa kati ya Rais Kenyatta na Bw Raila Odinga Matokeo yaliyotolewa kufikia sasa yanaonyesha Bw Kenyatta ana kura 7m naye Bw Odinga kura 5.6m. Bw Odinga anawania urais kwa mara ya nne. Kulikuwa na jumla ya vituo 40,883 vya kupigia kura kote nchini Katika matokeo ya vituo 36659 kati ya 40883: Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,461,933 (54.64%) Raila Odinga wa ODM ana kura 6,079,136 (44.51%) Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 353,389.

Bunge la Afrika Kusini limeshindwa tena kumuondoa Rais Zuma

Image
Rais wa Afrika Kusini amenusurika kwa mara nyingine katika kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa na bunge la nchi hiyo ambapo awamu hii ilikuwa ni ya tofauti kwani ilikuwa ni kura ya siri. Rais Zuma kwa vipindi  mfululizo ameshuhudia maandamano na kura za kutokuwa na imani zikipigwa kwa lengo la kumtaka ajiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa na upendeleo zinazomkabili. Kutokana na kura zilizopigwa jana na bunge la nchi hiyo, jumla ya kura hizo ni 384 huku waliosema hawana imani naye wakiwa 177, wenye imani wakiwa ni 198 na kura zilizoharibika ni 9. Kwa mujibu wa matokeo hayo, Wabunge 40 wa chama tawala, ANC wamepiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma hivyo kutaka ang’atuke. Viongozi mbalimbali wa ANC pamoja na wabunge wengine wa chama hicho, wametaka wabunge hao (40) wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kukisaliti chama. Muda mfupi baada ya bunge kutangaza matokeo hayo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu,...

Angalia Chama Cha NASA Cha RAILA ODINGA kilivyokataa Matoke Ya Kura, Kilivyotangaza Haya!

Image

Manji Alivyomkataa Wakili wa Chadema Mbele ya Mahakama...Kisa Kizima Hichi Hapa

Image
Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, Yusuf Manji jana alisema mbele ya mahakama kuwa hataki kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na kutaka abadilishe wakili kwa kile alichosema kuwa ni kutofautiana kwa itikadi za kisiasa. Manji ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania aliiambia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kwa maombi yake ya dhamana ambapo alishangaa yeye kama Diwani wa CCM kuwakilishwa na wakili ambaye ni mwanachama wa CHADEMA. Manji anayekabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi, baada ya kumkataa wakili huyo aliwatambulisha mawakili wengine wapya wawili ambao watamuwakilisha. Aidha, Mahakama Kuu jana ilitupilia mbali maombi ya dhamana ya Manji na kuanza mchakato wa kuipeleka kesi hiyo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa baada ya Manji kukubali pingamizi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuyaondoa mahakamani maombi ya dhamana. Mmoja wa mawakili wapya wanaomuwakilisha Manji, Alex Mgo...