Historia mpya aliyoweka Wizkid London
Muimbaji kutokea Nigeria Wizkid anayefanya vizuri na hit single ya wimbo wake Come Closer aliyomshirikisha msanii wa Marekani Drake , ameingia katika historia mpya kwa kuiwekea heshima Afrika baada ya kuweka rekodi England . Wizkid akiwa katika show nchini England katika jiji la London ameandika historia mpya ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kuwahi kufanya show Royal Albert Hall na kufanikiwa kujaza ukumbi wote. Naambiwa ukumbi wa Royal Albert Hall unauwezo wa kuingia mashabiki 5000 na Wizkid amefanikiwa kuuza tiketi zote na kukuta mashabiki wakimsubiri ukumbuni kwa zaidi ya saa mbili, kwa mujibu wa waandaaji unaambiwa tiketi za show hiyo zilimalizika siku mbili kabla ya show. Muimbaji kutokea Nigeria Wizkid anayefanya vizuri na hit single ya wimbo wake Come Closer aliyomshirikisha msanii ...