Matokeo ya urais ya wagombea wote wanane
mepakiwa mnamo 8:40 Kulikuwa na wagombea wanane katika kinyang'anyiro cha urais nchini Kenya. Matokeo kamili yalikuwa kama ifuatavyo: Ekuru Aukot 27,311 (0.18) Abduba Dida 38,093 (0.25) Cyrus Jirongo 11,705 (0.08) Japheth Kaluyu 16,482 (0.11) Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27) Michael Wainaina 13,257 (0.09) Joseph Nyagah 42,259 (0.28) Raila Odinga 6,762,224 (44.74) Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.2 na pia akapata angalau asilimia 25 ya kura katika kaunti 35. Mshindi wa urais huhitajika kupata asilimia 50 ya kura na kura moja zaidi, pamoja na angalau asilimia 25 katika kaunti 24. Baada ya kutangazwa mshindi, alitoa wito kwa mpinzani wake Raila Odinga, ambaye muungano wake uliyakataa matokeo, aungane naye kufanya kazi kwa maslahi ya taifa. ""Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamo...