Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya: Klabu sita za Uingereza kwenye droo Uefa
Haki miliki ya picha Image caption Real Madrid walilaza Juventus kwenye fainali msimu uliopita na kuwa klabu ya kwanza kuhifadhi kombe hilo Klabu sita kutoka Uingereza, tano za England na moja ya Scotland, zinasubiri kwa hamu droo ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambayo itafanyika Alhamisi saa 17:00 BST (saa moja jioni Afrika Mashariki) mjini Monaco. Mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea, Tottenham waliomaliza wa pili na Manchester City waliomaliza wa tatu wote wamo kwenye droo. Watajumuika pia na washindi wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Manchester United, pamoja na Liverpool waliofuzu kupitia hatua ya muondoano sawa na mabingwa wa ligi ya Scotland Celtic. Mechi za hatua ya makundi zitaanza kuchezwa 12-13 Septemba. Mara ya mwisho wa klabu sita za Uingereza kufika hatua ya makundi ilikuwa mwaka 2007-08 pake klabu za England Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal zilifuzu pamoja na klabu za Scotland Celtic na Rangers. United wakiwa na Sir Alex Ferguson...